VIDEO: Mafuriko yafukua makaburi 20 Mwanza

Muktasari:

  • Makaburi zaidi ya 20 yaliyopo eneo la Mswahili ambayo yanatumiwa na Waislam Kata ya Mkuyuni jijini Mwanza yamefukuliwa kutokana mvua kubwa iliyonyesha jana Ijumaa jijini humo.

Mwanza. Mvua kubwa iliyonyesha jana Ijumaa Oktoba 18, 2019 jijini Mwanza nchini Tanzania umesababisha makaburi zaidi ya 20 kuyafukua.

Makaburi hayo ni yale yanayotumiwa na Waislam yaliyopo eneo la Mswahili, Kata ya Mkuyuni jijini Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Oktoba 19, 2019 wakati wa shughuli ya kutafuta mabaki ya miili, Ofisa  Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni, Ibrahim Joseph amesema taratibu za kusitiri mabaki hayo zitafanyika baadaye kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislam.

Mvua hiyo ilinyesha kwa zaidi ya saa moja jana Ijumaa mchana kuanzia saa 7:45 mchana hadi saa 9:14 alasiri pia ilisababisha mto Mirongo inayopita katikati ya jiji kufurika na kusomba bidhaa zilizopangwa kwenye mabaraza ya maduka ya jumla na rejereja katika mitaa ya Liberty na Uhuru jijini humo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi