Mafuriko yaua watu saba Korogwe

Muktasari:

  • Kaya zaidi ya 300 za wakazi wa Wilaya ya Korogwe hazina mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kujaa maji kutokana na mvua inayoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo mkoani Tanga.

Korogwe. Watu saba wamefariki dunia na kaya zaidi ya 300 Wilayani Korogwe hazina mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kuanguka na zingine kujaa maji kutokana na mvua inayoendelea kunyesha wilayani humo.

Akizungumza na Mwananchi usiku huu, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Edward Bukombe amesema vifo hivyo vimetokea katika vijiji vya Bungu, Dindira na Vingo, wilayani Korogwe.

Akizungumzia hali hiyo mapema mchana wa leo Jumatano Oktoba 9,2019, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa alisema mafuriko hayo yameathiri maeneo ya

Majimbo ya Korogwe Mji na Korogwe Vijijini.

Ameyataja maeneo yaliyoathirika ni Masuguru, Chuo cha Ualimu cha Early Education kilichopo Mbeza, Soko la Manundu, Kilole na Mgombezi.

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mji, Mary Chatanda amesema kwa kushirikiana na viongozi wengine, wamelazimika kufanya kazi ya kuwakoa watu ambao nyumba zao zimezingirwa na maji ya Mto Pangani na Mto Mbeza.

Amesema wamefanikiwa kuwahamishia kwenye maeneo ambayo hayana mafuriko.

“Tupo katika harakati za kuwahamisha wananchi, hali ni mbaya sana

Nyumba za kuishi, majengo ya shule na ya taasisi nazo zimejaa maji ila kwa sasa tunawaokoa watu kwanza,” amesema Chatanda.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,Gwakisa alisema idadi kamili ya waliokosa

mahala pa kuishi pamoja na madhara yaliyotokana na mafuriko hayo

yatatolewa baada ya kamati ya ulinzi na usalama pamoja nay a maafa

kukaa na kufanya tathimini.

“Bado tunakusanya taarifa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilayani hapa

halafu tutakutana kamati za ulizni nay a maafa kufanya tathmini ya

madhara yaloiyotokea”alisema Gwakisa.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Tanga, Alfread Ndumbaro amewataka madereva kutotumia barabara za Old Korogwe, Magoma Songea

Kilole na Kwasunga kwa kuwa madaraja yake yameathirika.

“Madereva na wananchi wasubiri kwanza mafuriko yapungue ili kusitokee

madhara kwa kuwa madaraja ya Mto Msangazi  pale ilipotokea ajali ya No

Challenge miaka ya nyuma na kuua watu wengi,maji yanapita juu na njia

Haionekani na Magoma daraja limemegwa upande,” amesema Ndumbaro.

Amesema timu ya wataalamu kutoka Tanroads imesambazwa katika maeneo hatarishi kwa ajili ya kutoa msaada.