Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha mbunge CCM

Wednesday January 15 2020

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge, Job Ndugai kufuatia kifo cha mbunge wa Newala Vijijini (CCM), Rashid Akbar kilichotokea leo Jumatano Januari 15, 2020 mkoani Lindi.

Taarifa iliyotolewa leo na mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa katika salamu hizo, Magufuli ameelezea kuhuzunishwa na kifo hicho.

“Spika naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu, wabunge, wananchi wa Newala vijijini na wote walioguswa na msiba huu, nawaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi” amesema Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM.

Advertisement