Rais aliyekaa madarakani miaka 30 Misri, Hosni Mubarak afariki dunia

Muktasari:

Kiongozi huyo wa zamani wa Misri alimembwa na umauti leo katika hospitali moja alipokuwa amelazwa kwa ajili ya kufanyiwa upasaji.

Misri. Kiongozi wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak amefariki dunia.

Televisheni ya taifa ya Misri ilisema kuwa Mubarak aikufa katika Hospitali moja iliyopo mjini Cairo, Misri alipokuwa amelazwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Hata hivyo, hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusiana na upasuaji huo.

Hosni Mubarak alikuwa kiongozi wa Misri aliyedumu kwa miongo mitatu madarakani kabla ya  mwaka 2011 kulazimishwa na jeshi la nchi hiyo kujiuzulu.

Hatua hiyo ilifuatia maandamano ya nchi nzima yaliyodumu kwa siku 18.

Televisheni ya taifa imetangaza kuwa Mubarak amefariki akiwa na umri wa miaka 91. Muda wote wa utawala wake, alikuwa mshirika wa karibu wa Marekani, akipambana vikali dhidi ya uasi wa makundi ya itikadi kali za kiislamu na mlinzi wa mkataba wa amani kati ya Misri na Israel. Lakini kwa maelfu na maelfu ya Wamisri vijana walioandamana kwa siku 18 mabarabarani katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo na kwingineko mwaka 2011, Mubarak alikuwa kama farao.