Tundu Lissu azungumzia ubunge wake

Friday June 28 2019

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Baada ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kusema Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amepoteza  sifa za kuendelea kuwa mbunge, Lissu amesema atakwenda mahakamani.

Lissu amesema hayo leo usiku Ijumaa Juni 28, 2019 wakati akizungumza na Mwananchi kwa simu akiwa Ubelgiji, amesema tangu aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa Area D jijini Dodoma Septemba 7, 2019 amekuwa akipata matibabu nje ya nchi.

Amesema kwa hatua ya sasa, “Nitawasiliana na wanasheria wangu haraka iwezekanavyo ili kuona cha kufanya lakini Septemba 7 (mwaka huu) ambayo nilikwisha kusema nitarudi   sitabadili, nitarudi na alichokifanya Ndugai ni kukoleza mjadala.”

Leo jioni Juni 28, 2019, Spika Ndugai ameliambia Bunge hilo kuwa amewandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha kuwa kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kipo wazi.

Amesema hatua hiyo inatokana na Lissu ni kutojaza taarifa za mali na madeni na sababu ya pili kutokutoa taarifa kwa Spika mahali alipo.

Hata hivyo, katika mazungumzo na Mwananchi Lissu amezungumza kwa kina akitoa sababu nne akimjibu Spika Ndugai, unataka kujua ni sababu zipi, usikose gazeti la Mwananchi kesho Jumamosi Juni 29, 2019. Humo utajua kasema nini kuhusu kurejea nchini na mengine mengi.

Advertisement

 

Advertisement