Atumia wimbo wa Davido kupiga mkwanja

Muktasari:
- Emzy Pondeck amejipatia umaarufu unaomfanya apige pesa ndefu kwa kufanya 'show' ya cover ya wimbo uitwao 'Kante' wa mwanamuziki Davido
Kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii Bongo kutikisa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ngoma za wasanii wengine kwa kuzifanyia cover, ndivyo ilivyotokea kwa kijana kutoka Nigeria, Emmanuel Ogbole, maarufu kwa jina la Emzy Pondeck.
Emzy amejipatia umaarufu unaomfanya apige pesa ndefu kwa kufanya 'show' ya cover ya wimbo uitwao 'Kante' wa mwanamuziki Davido uliopo kwenye albamu ya Timeless.
Kibogo bongo pia, wapo wasanii walioanza kufuatiliwa baada ya kuanza kufanyia cover nyimbo za wasanii maarufu, kati ya wasanii hao wakiwamo Dayoo, Anjela.
‘Kante' ni wimbo wa kumi kati ya nyimbo 16, kwenye albamu ya Davido ya 'Timeless' iliyotoka mwaka 2023, huku nyingine zikiwa ni 'Over Dem', 'Godfather', 'Unavailable' na 'Away.'
Hadi sasa wimbo huo kwenye YouTube Channel ya Davido unawatazamaji milioni sita ukiwa na miezi tisa tangu utoke.