Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Angel Nyigu ana jambo lake na Rayvanny

Muktasari:

  • Nyigu ameiambia Mwananchi kuwa ameonekana kwenye video nyingi lakini video ya wimbo wa Makulusa ulioimbwa na Rayvanny akishirikiana na DJ Maphorisa & DJ Buckz ndiyo uliomtambulisha

Mnenguaji, Angel Nyigu amefichua kwamba hana ndoto wala mpango wa kuwa mwanamuziki lakini amemtaja msanii wa kundi la WCB, Raymond Shaban 'Rayvanny' kuwa ndiye aliyemfanya ajulikane.

Nyigu ameiambia Mwananchi kuwa ameonekana kwenye video nyingi lakini video ya wimbo wa Makulusa ulioimbwa na Rayvanny akishirikiana na DJ Maphorisa & DJ Buckz ndiyo uliomtambulisha.

"Kila video niliyoifanya na kuonekana ina matokeo yake lakini kazi ya Makulusa ndiyo imenifanya nikajulikana na kuwashawishi wasanii wengi wakubwa kutamani kufanyakazi na mimi," amesema na kuongeza;

"Nimefanya kazi na wasanii wengi wakubwa na nafurahia wanavyoimba lakini kwa upande wangu sipo tayari kuingia kwenye sanaa hiyo kwani sina utayari na kuimba ila nitapambana niweze kucheza 'style' zote kwa sababu ndiyo kazi nimeichagua." Amesema Nyigu.