Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Billnass afungukia ishu yake, mkewe na Diamond

Muktasari:

  • Hayo ameyasema leo Septemba 13, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Huku akijibu maswali wanayojiuliza mashabiki kuwa kwa wakati huu ambao tamasha la Wasafi Festival na Nandy Festival yanaendelea lipi atalolipa kipaumbele zaidi

Dar es Salaam, Mwanamuziki William Lyimo 'Billnass' amesema kabla ya kwenda kwenye tamasha lolote ambalo atakuwa amealikwa kitu cha kwanza ambacho huwa anaangalia maslahi ya tasnia kabla ya kuangalia ya kwake binafsi.

Hayo ameyasema leo Septemba 13, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Huku akijibu maswali wanayojiuliza mashabiki kuwa kwa wakati huu ambao tamasha la Wasafi Festival na Nandy Festival yanaendelea lipi atalolipa kipaumbele zaidi.

"Kuna vitu vingine nikivifanya najua naweza kunufaika navyo lakini naweza kuacha kufanya kama vitakuwa havina tija na maslahi kwenye tasnia kwa ujumla kwa hiyo matamasha yote hayo malengo yao ni kuhakikisha sekta ya burudani inaendelea kukua.

"Watu wanawekeza na kutumia muda wao kuandaa matamasha kwa hiyo sisi kama wasanii lazima tuhakikishe matamasha yanafanikiwa na tunahitaji kuwa na matamasha mengi zaidi,"amesema.

Amesema hata akiwa kwenye kazi hasa tamasha la Nandy Festival ambalo linaandaliwa na mkewe Nandy huwa anafanya kazi kama msanii na siyo kama mume.

"Nandy Festival nafanya kama msanii mwingine kwa sababu hii ni biashara mimi pia nina team, dansa tutashiriki tamasha lolote ambao tutaona linatija kwetu kibiashara na tasnia kwa ujumla.

"Kwa sababu natamani kuona kuna matamasha mengi na naangaia namna gani ninaweza kujigawa mimi na Wasafi tuna mazungumzo mazuri ratiba yangu wanaijua, naheshimu mkataba wangu,"amesema.