Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chanzo Msamiati kutumia lugha ya Kinyakyusa kwenye nyimbo zake

Muktasari:

  • Lakini hilo limekuwa tofauti kwa Freddy Benny Mbetwa, anayejulikana kwa jina la Msamiati, aliyejiwekea alama ya kipekee katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kwa kutumia lugha ya Kinyakyusa katika nyimbo zake. 

Wasanii wengi wanaotamani kuvuka mipaka na kufanikiwa kimataifa, hufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuiga ladha na lugha za mataifa mengine ili kuyafikia mafanikio hayo.

Lakini hilo limekuwa tofauti kwa Freddy Benny Mbetwa, anayejulikana kwa jina la Msamiati, aliyejiwekea alama ya kipekee katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kwa kutumia lugha ya Kinyakyusa katika nyimbo zake. 

Nyimbo zake maarufu, kama vile Malafyale (ambayo ina maana ya Mfalme kwa Kinyakyusa), Ndagha (asante), na Mwaisa (rafiki), zimevutia mashabiki kutoka Afrika Mashariki kutokana na midundo ya kuvutia na matumizi ya lugha hiyo.

Licha ya dhana ya awali kwamba kuingiza lugha ya kiasili katika muziki wake kungewalenga hasa mashabiki wa rap wa ndani, mbinu ya Msamiati imevunja matarajio, na kuvutia mashabiki na wasanii zaidi hadi nje ya mipaka, hususani Kenya, Uganda, na sehemu zingine za Afrika, kama anavyoiambia Mwananchi.

Amezaliwa na kukulia Tukuyu, Mbeya, safari ya muziki ya Msamiati ilianza tangu akiwa shule.

"Nilianza kufanya muziki nikiwa bado shuleni. Tukiwa Wakristo, tulikuwa na desturi nyumbani ya kuimba nyimbo za kidini za kitamaduni baada ya sala," amesema.

Midundo ya lugha yake ya asili umeweka msingi wa utambulisho wake kwenye muziki. Alipokuwa akijitafuta kwenye aliwafuatilia magwiji wa hip-hop wa Tanzania kama Professor Jay, Ngwair, Juma Nature, na Joh Makini. Msamiati anasema alivutiwa na ubunifu wao.

"Joh Makini alikuwa mmoja wa wasanii walionipa hamasa kuja Dar es Salaam kupitia wimbo wake maarufu 'Chochote Popote," anasema.

Kwa mujibu wake, wasanii hawa walikuwa kama walimu waliomsaidia jinsi ya kuunda nyimbo zake na kuchagua maneno.

"Nilikuwa naamini na kuota kwamba Dar es Salaam ilikuwa mahali pekee pa kutimiza ndoto zangu." Alipofika Dar es Salaam, alirekodi wimbo wake wa kwanza, Moja Moja, ambao anasema una nafasi maalum moyoni mwake.

"Wimbo huo ulikuwa na maana kubwa katika maisha yangu ya muziki. Ulifanya nifikie maono yangu ya kisanii na kuwasilisha mawazo na hisia zangu kama nilivyokuwa nikifikiria. Shukrani kwa utaalamu wa mtayarishaji Marco Charlie, wimbo huu ulikuwa na hatua kubwa mbele kwangu" anaeleza.

Anaongeza kwamba kuunda wimbo huu ilikuwa ni jambo la kusisimua kwa sababu alikuwa ameweka lugha ya Kinyakyusa katika kazi yake. "Ni jambo ambalo halijawahi kufanywa kabla, hasa katika soko la muziki wakati huo," anaeleza.

Anakumbushia mapokezi ya watu juu ya wimbo huo kila walipokuwa wakiusikia redioni

"Nakumbuka wimbo ulikuwa ukichezwa kwenye kila kituo cha redio, watu wakinipigia simu kila kona. Wengine walishangaa kunisikia nikitumia Kinyakyusa katika muziki wangu, lakini kwangu, hii ilikuwa mwanzo" anasema.

Akizungumzia uamuzi wa kuingiza lugha yake ya asili, Kinyakyusa, katika muziki wake, Msamiati anasema anaiona kama maendeleo ya asili yaliyochochewa na uhusiano wake na urithi wake wa kitamaduni.

"Uamuzi wa kuanza kutumia lugha yangu ya asili katika muziki wangu ulitokana na nyimbo tulizokuwa tukiimba wakati wa sala nikiwa mtoto," anaeleza Msamiati.

Hata hivyo, Msamiati anaona matumizi ya lugha yake ya asili kama zana yenye nguvu ya kuhifadhi utamaduni na kufikia ulimwengu.

"Linapokuja suala la lugha, ni jambo linalokuja kwa asili kwangu, na ndilo linalonifanya niwe tofauti na wasanii wengine" anasisitiza.