Jiongeze: Sanaa ina warembo wengi kuliko wasanii
Muktasari:
- Siku hizi wengi huingia kwenye sanaa siyo kwa kuipenda sanaa. Hawana huba wala haba na fani. Wapo kwa kiu ya kutazamwa na wengi. Ndo maana ubunifu ni jambo gumu kwao wakijali sura na shepu
Dar es Salaam. Unamkumbuka yupi katika sanaa ya uigizaji. Aliyetamba zamani na sasa yupo nje ya sanaa. Vipi juu ya Nora, binti mrembo kabla ya ‘filta’ na ‘mekapu’ zinazowabeba waigizaji wa leo?
Siku hizi wengi huingia kwenye sanaa siyo kwa kuipenda sanaa. Hawana huba wala haba na fani. Wapo kwa kiu ya kutazamwa na wengi. Ndo maana ubunifu ni jambo gumu kwao wakijali sura na shepu.
‘Samtaim’ hii fani ni huzuni. Wapo wenye dhamira na vipaji kweli. Na ambao hawana wito bali kwa mizuka ya mjini. Ni kama kuna kundi flani halitaki wasanii halisi watambe, wametaka kila kitu.
Hawajali juu ya vipaji na weledi wa fani. Vipi mafunzo kwa jamii kama kusudio la sanaa? Enzi za Kibakuli na Nyamayao kipi wewe unakumbuka? Vishoka wa sanaa wamewapoteza wengi.
Tunakosa maigizo ya uhalisia, vipaji vya uhakika na hadithi za kibunifu zenye kutoa funzo kwa jamii. Kaole iliyomtoa Dr Cheni, Swebe, Ben, Kisa, Mainda, Johari, Kemmy, Mashaka (RIP).
Splendid ya Billy na Migomba, Mau, Dude na Chekibudi. Hawa walifanya sanaa bila wawekezaji na muitikio mkubwa, ila waliacha alama muhimu za kukumbukwa. Kuna kasoro zenye kasoro sasa.
Kuna Waridi, Aisha, Bishanga na Mjomba Fujo. Maisha yapo kasi sana sanaa ina warembo kuliko wasanii. Frank Mwigongi, Jack wa Chuzi, Mikala na Jini Kabula. Tumebaki na Elizabath Michael tu?