Jiongeze: Usilete stori hizi mkienda viwanja kula bata
Marafiki wakila bata huku wakipiga stori. Picha na Akili Mnemba
Muktasari:
- Piga stori zingine, mbona ziko nyingi tu. Kujielezea sana shule yako ni ushamba fulani hivi, dizaini kama hujiamini so lazima ujivishe nyota. Unaboa.
Dar es Salaam. Ukienda kijiweni, pub au nyama choma achana na stori za sijui umesoma wapi hadi wapi, mara sijui una madigirii mangapi.
Piga stori zingine, mbona ziko nyingi tu. Kujielezea sana shule yako ni ushamba fulani hivi, dizaini kama hujiamini so lazima ujivishe nyota. Unaboa.
Tembea na keshi mfukoni kama vipi, stori za kadi yangu ya benki imegoma siyo ishu. Punguza mambo yako ya kuvaa sana kipapaa. Sometimes ibuka na pensi na jinsi tu mwana.
Acha kukesha nje mfululizo, iwe umeoa, una mpenzi au upo upo.
Kikanuni kabisa usikae nje hadi usiku wa manane siku tatu mfululizo labda uwe na mchongo wa maana sana. 'Ai miini' wa maana sana.
Epuka sana mchezo wa kujipiga tattoos. Kuna watu wamekosa wake au 'dili' kwenye 'laifu' kisa hizo mambo sanuka mwana.
Bia moja au glasi moja ya 'waini' baada ya mlo wa usiku haiwezi kuvuruga akili na bajeti.
Kama hutaki, kunywa majuisi basi na soda zako ujaze magonjwa mwilini.
Kwanza tambua kuwa hakuna watu wenye roho safi na umoja kama wapiga monde. Wana kaumoja flani hivi kama sisimizi.
Mtoto wa kiume hapigi selfie ovyo ovyo na kubinua midomo wala kulamba lipsi.
Piga 'selfii' kwenye 'ishu' za muhimu, familia hivi au mrembo mkali. Umenisoma?
Ukiweza miliki hata panga au nyundo ghetto kwako, maana bastola najua ni ngumu.