Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joel Lwaga, Moses Bliss kukiwasha The Rising Fest

Muktasari:

  • Tamasha hilo pia litatoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao, kujifunza na kuunganishwa na wadau mbalimbali wa sekta za ubunifu, huku akisisitiza kuwa dhamira yake ni kuacha alama ya kudumu katika jamii.

Dar es Salaam. Mwimbaji nyota wa muziki wa injili nchini, Joel Lwaga, anatarajiwa kushiriki jukwaa moja na msanii wa kimataifa kutoka Nigeria, Moses Bliss katika tamasha la The Rising Fest litakalofanyika Agosti 15, 2026, kwenye Viwanja vya Klabu ya Gofu ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo, lenye kaulimbiu ya "Faith Without Borders" (Imani Bila Mipaka), litawakutanisha maelfu ya vijana, familia, wanafunzi wa vyuo na wadau mbalimbali kwa siku nzima ya muziki wa injili, ibada, ubunifu, mitindo pamoja na shughuli za kijamii.

Mbali na Joel Lwaga na Moses Bliss, jukwaa hilo pia litapambwa na Neema Gospel Choir sambamba na wasanii chipukizi, huku waandaaji wakiahidi burudani yenye ujumbe wa matumaini, imani na mabadiliko chanya kwa vijana.

Waandaaji wamesema The Rising Fest imekusudiwa kuwa zaidi ya tamasha la muziki, kwa kulenga kukuza vipaji vya ubunifu, kuhamasisha ujasiriamali na kuendeleza maadili mema kupitia sanaa na teknolojia.

Akizugumza na Mwananchi leo Jumamosi, Julai 25, 2026, Mwanzilishi wa Color Creative House, Karolyn Klaire amesema tamasha hilo lina lengo la kuanzisha enzi mpya ya utamaduni wa vijana kwa kuunganisha burudani na imani katika mazingira salama yanayochochea ubunifu na mafanikio.

"The Rising Fest inavuka mipaka ya burudani; ni vuguvugu linalowezesha kizazi kijacho kupitia muunganiko wa muziki, teknolojia, mitindo na utamaduni," amesema Klaire.

Amesema tamasha hilo pia litatoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao, kujifunza na kuunganishwa na wadau mbalimbali wa sekta za ubunifu, huku akisisitiza kuwa dhamira yake ni kuacha alama ya kudumu katika jamii.

"Hili ni zaidi ya tamasha; ni vuguvugu linalounda mustakabali wa utamaduni wa vijana Afrika Mashariki. Tunakaribisha wadau kushirikiana nasi kuwekeza kwa kizazi kijacho na kuinuka pamoja (Rise Up)," amesema.

Tamasha hilo litafanyika kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 5:00 usiku. Tiketi zitauzwa kuanzia Sh10,000 kwa watoto, huku tiketi za mapema kwa watu wazima zikiuzwa kwa Sh20,000.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya tamasha hilo, shabiki wa muziki wa Injili, Janeth Mbonia anasema wanatarajia kupata burudani safi kwa kuwa waandaaji wamejipanga kuhakikisha washiriki wanapata uzoefu wa kipekee.

Kwa upande wake, Joseph Mwangaamesema ushiriki wa Joel Lwaga na Moses Bliss unaonesha dhamira ya tamasha hilo kuwaleta pamoja wasanii wa ndani na wa kimataifa kwa lengo la kuhamasisha vijana kupitia muziki wa injili.

Naye Karolyn Klaire, mwanzilishi wa Color Creative House, amesema The Rising Fest si tamasha la muziki pekee bali ni jukwaa la kukuza ubunifu, ujasiriamali na maadili kwa vijana.