Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamati ya mazishi ya Mr Ibu yaomba msaada

Muktasari:

  • Kufuatia barua hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kamati Kuu Diamond, katibu Ijele na Rais wa Chama cha Waigizaji cha Nigeria, Emeka Rollas imelenga kuomba msaada wa kifedha ili kusaidia kukamilisha mazishi hayo kama yalivyopangwa.

Baada ya kutangaza tarehe ya mazishi ya mwigizaji kutoka Nigeria Mr Ibu, mwenyekiti aliyeteuliwa kusimamia mazishi ya mwigizaji huyo Monday Diamond A. JP (Odoziobodo) ametoa waraka wa kuiomba serikali na wadau mbalimbali kuchangia fedha kwa ajili ya mazishi hayo.

Kufuatia barua hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kamati Kuu Diamond, katibu Ijele na Rais wa Chama cha Waigizaji cha Nigeria, Emeka Rollas imelenga kuomba msaada wa kifedha ili kusaidia kukamilisha mazishi hayo kama yalivyopangwa.

Ikumbukwe kuwa Mr Ibu (62) amefariki dunia Machi 2, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Evercare iliyopo nchini Nigeria, na anatarajiwa kuzikwa Juni 28, 2024 katika mji aliozaliwa wa Amuri, katika eneo la serikali ya Mtaa wa Nkanu Magharibi katika Jimbo la #Enugu.

Mazishi ya mwigizaji huyo yanapangwa kuwa ya kihistoria kwa kuwepo kwa sherehe ya siku tano ambapo hafla hiyo itaanza Juni, 25 kutakuwa na mechi maalumu, Juni 26 Usiku wa Mr Ibu kutakuwa na mishumaa pamoja na burudani ya moja kwa moja.

Juni 27 kutakuwa na ibada maalumu nyumbani kwao huko Eziokwe Amuri, ibada ya mazishi ikifanyika Juni 28 na sherehe hizo zitatamatika Jumapili Juni 30 ambapo familia itatoa shukrani kwa kanisa, marafiki na watu wengine waliohudhuria katika hafla zote za siku tano.

Mr Ibu watu wengi walimtambua kupitia filamu zake kama The Collaborator, My Chop Money na nyingine nyingi akiwa na Aki na Ukwa.