Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Ibraah na Harmonize kila mwaka ilikuwa sherehe

Muktasari:

  • Akiwa ametoa EP tatu, Steps (2020), Karata 3 (2021) na Air Piano (2024) pamoja na albamu moja, The King of New School (2022), Ibraah a.k.a Chinga amejizolea umaarufu kwa tungo zake zinazohusu mapenzi na starehe.

Dar es Salaam. Miaka yake mitano ndani ya Bongofleva imetosha kuonyesha ukubwa wa kipaji chake, Ibraah, mwanamuziki wa zamani wa lebo ya Konde Music Worldwide ni miongoni mwa waimbaji wapya wanaofanya vizuri.

Akiwa ametoa EP tatu, Steps (2020), Karata 3 (2021) na Air Piano (2024) pamoja na albamu moja, The King of New School (2022), Ibraah a.k.a Chinga amejizolea umaarufu kwa tungo zake zinazohusu mapenzi na starehe. Mfahamu zaidi.

1. Ibraah alianza kuimba akiwa shule msingi huko Mtwara, kipaji chake kikamfanya kuwa msanii bora wa shule, msanii bora wa kata na mwaka 2014 akawa msanii bora wa wilaya (Tandahimba) kati ya wasanii 36 waliokuwa wanawania nafasi hiyo.

2. Baadaye Ibraah alikuwa Dar es Salaam na kuanza kazi umachinga na ndio sababu ya kujiita 'Chinga', alikuwa anauza CD, huku akiwa na ndoto kubwa ya kufanya muziki ila hakujua wapi pa kuanzia hadi kuja kufanikiwa.

Aliposikia Harmonize amefungua lebo, Konde Music akawa kila mara anaenda kugonga hodi katika ofisi hiyo kuomba nafasi ya kusainiwa ila hakufanikiwa kukutana na Harmonize.

3. Aliyekuwa prodyuza wa Harmonize, Bonga alipokutana na Ibraah alivutiwa na uwezo wake kimuziki, akamshauri akatafute fedha ya kurekodi na mpango wa kuchukuliwa na Konde Music asiufikirie sana.

Ibraah akakubali wazo la Bonga, hivyo akasaka fedha ya kurekodi hadi kuipata na kweli akarekodi, punde tu DJ wa Harmonize, Seven aliposikia wimbo huo akaupenda na kwenda kumsikilizisha Harmonize ambaye alivutiwa nao na kukubali kumsaini.

4. Hivyo Ibraah ndiye msanii wa kwanza kusainiwa Konde Music Worldwide kisha wakafuata wengine kama Country Wizzy, Cheed, Killy, Anjella na Young Skales kutokea nchini Nigeria.

5. Mnamo Aprili 11, 2020 ndipo Konde Music walitangaza kumsaini Ibraah aliyetambulishwa na EP yake, Steps (2020) ikiwa na nyimbo tano, huku akiwashirikisha Harmonize pamoja na wasanii wawili wa Nigeria, Joeboy na Skibii.

6. Harmonize alimkuta Ibraah amesharekodi wimbo, One Night Stand (2020) akaupenda na kuomba kuongeza vesi yake kitu ambacho Ibraah alikubali na ulipotoka ukafanya vizuri  na hadi sasa video yake ikiwa na 'views' zaidi ya milioni 20 YouTube.

7. Tangu ameanza muziki hadi kuachana na Konde Music hivi karibuni, Ibraah hajawahi kushinda tuzo yoyote zaidi ile aliyopewa na kipindi cha Empire cha E FM Radio kama Msanii Bora Chipukizi 2020.

8. Albamu ya kwanza ya Ibraah, The King of New School (2022) haikushirikisha msanii yeyote wa Konde Music, waliopata nafasi ni wale kutoka nje ya lebo hiyo ambao ni Maud Elka, Christian Bella, L.A.X, Waje, AV, Roberto na Bracket.

9. Jina alilopewa na wazazi wake ni Ibrahim Abdallah Nampunga, hivyo hilo la Ibraah amelitoa huko ila kwenye Bongofleva alikuta kina Ibraah wenzake wawili .

Kuna Ibra Nation aliyetolewa na Tanzania House of Talent (THT) kupitia wimbo wake, Nilipize (2017), pia kuna Ibra Da Hustler wa kundi la Nako 2 Nako Soldiers kutokea Arusha ambalo liliundwa na wasanii wanne.

10. Tangu alipojiunga na Konde Music mwaka 2020, kila mwaka Ibraah alikuwa anatoa wimbo na Harmonize na hii ndiyo maana ya kila mwaka Ibraah na Harmonize walikuwa na sherehe. Tayari wameshirikiana katika nyimbo tano ambazo ni One Night Stand (2020), Addiction (2021), Mdomo (2022), Tunapendeza (2023) na Dharua (2024)