Marioo, Diamond, Harmonize, Zuchu waongoza Spotify 2024
Muktasari:
- Mapema leo Desemba 5, 2025, Spotify imetaja kuwa kati ya wasanii 10 waliosikilizwa sana Tanzania, wanne ni wasanii wa Tanzania na 6 (sita) kutoka nchi nyingine Barani Afrika
Dar es Salaa. Zikiwa zimebaki wiki kadhaa kuupindua mwaka 2024 na kuingia 2025, mtandao wa kuuza na kusikiliza muziki wa Spotify umeshusha orodha ya wasanii wanaosikilizwa zaidi kutoka Tanzania.
Mapema leo Desemba 5, 2025, Spotify imetaja kuwa kati ya wasanii 10 waliosikilizwa sana Tanzania, wanne ni wasanii wa Tanzania na 6 (sita) kutoka nchi nyingine Barani Afrika.
Kati ya wasanii hao ni pamoja na Marioo, Diamond Platnumz, na Harmonize. Huku Alikiba akishika nafasi ya 10.
Aidha mbali na hilo pia mtandao huyo umeorodhesha albamu zilizosikilizwa zaidi ni pamoja na “The Kid You Know” – Marioo, “Visit Bongo”- Harmonize, “Therapy”- Jay Melody, “Most People Want This”- Navy Kenzo, na “Made For Us” yake Harmonize.
Hata hivyo, kupitia orodha hiyo imeonesha nyimbo 10 zilizosikilizwa ndani ya Tanzania na Afrika kote huku orodha hiyo ikiongozwa na wimbo wa Hakuna Matata wa Marioo.
Nyimbo nyingine ambazo zimesikilizwa zaidi ni pamoja na “Mapoz (ukiwashirikisha Mr Blue & Jay Melody)” – Diamond Platnumz, na “Buruda” – Jaivah, : “Zawadi (Dadiposlim) – Zuchu, “Dharau” – Ibrah, na “Nisiulizwe” – Jux. Huku wasanii waliosikilizwa sana ni Marioo, Diamond Platnumz, Jay Melody, na Jaivah.
Hata hivyo, kwa upande wa wasanii wa kike nchini mwanamuziki anayetamba na wimbo wa ‘Wale Wale’ aliyomshirikisha Diamond, Zuchu ametajwa kuongozwa kusikilizwa katika mtandao huo.
Zuchu ametajwa kuwa kinara kwa wasanii wa kike kutokana na kuendelea kutia alama katika muziki wa Bongo Fleva huku wasanii wengine wanaosikilizwa zaidi ni pamoja na Nandy na Phina.
Tangu kutambulishwa kwake katika lebo wa WCB mwaka 2021 Zuchu amekuwa akiachia ngoma ambazo zinapenya zaidi ndani na nje ya nchi ikiwemo Sukari, Siji, Antena, Zawadi, Napambana na nyinginezo.
Mbali na kutajwa kuwa msanii anayesikilizwa zaidi lakini pia nyimbo zake mbili zimeripotiwa kusikilizwa zaidi ikiwemo Siji aliyomshirikisha Toss na Zawadi aliyomshirikisha Dadiposlim.