Faras: Usafiri mtandaoni unavyowazawadia wateja wake

Faras ni kampuni inayotoa huduma za usafiri mtandaoni maarufu kama Taxi-mtandao, imeleta mapinduzi katika tasnia ya usafiri nchini Tanzania kupitia mpango wake wa kipekee wa uaminifu wa kuwazawadi wateja wake na Farasmiles.

Farasmiles ni mfumo wa tuzo ambazo zina thamani sawa na fedha ambazo huzawadiwa kwa wateja kwa njia mbalimbali anapopakua programu ya Faras na kujisajili, anapokea zawadi ya Farasmiles 3,000/=. Kila safari inayofanywa na mteja huongeza asilimia 10 ya gharama ya safari kwenye akaunti yake.

Pia, kuna malengo ya kila siku na kila wiki. Kwa mfano, mteja anayefanya safari nne kwa siku anapokea Farasmiles 1,000 ili kufikia malengo ya safari kwa wiki kunaweza kumletea mteja zawadi ya hadi 20,000.


Faras pia inajivunia huduma yake ya simu ya bure inayopatikana masaa 24, inayompa fursa mteja kutoa ripoti au kuomba usafiri bila kuhitaji intaneti. Huu ni mkakati mzuri katika mazingira ya Tanzania ambapo kipato cha kila mwananchi ni cha chini.

Kampuni hiyo inaendesha shughuli zake nchini Tanzania, na mpango huu wa simu ya bure unahakikisha huduma zao zinapatikana kwa kila mtu, hata wale wasio na simu za kisasa. Siyo tu kwa watumiaji wa simu za kawaida bali pia watumiaji wa simu za kisasa ambao mara kwa mara hawana data ya intaneti ya kutumia programu ya Faras.

Mpango huu wa zawadi wa Farasmiles na huduma ya simu ya bure vinaweka Faras mbele katika soko la usafiri wa ndani, na tunatarajia kuona jinsi wanavyoendelea kubadilisha na kuboresha tasnia hii muhimu nchini Tanzania.