Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lindi yauza mbaazi za Sh38 bilioni

Wakulima wa Zao la mbaazi wakifungua sanduku kwa kuanza kwa mnada.Picha na Bahati Mwatesa

Muktasari:

  • Zaidi ya Sh38 billioni zimekusanywa katika msimu wa mbaazi wa 2023 kwa minada 11 iliyofanyika katika Mkoa wa Lindi.

Lindi. Wakati msimu wa zao la mbaazi wa 2023 ukiisha, jumla Sh38 billion zimekusanywa kutokana na mauzo ya zao hilo yaliyofanyika katika minada 11 mkoani Lindi.

Aidha imeelezwa kuwa, katika mnada wa mwisho, ulioongozwa na Chama Kikuu cha Lindi Mwambao, jumla ya tani 200 ziliuzwa kwa Sh1, 905 kwa kilo.

Akizungumza na Mwananchi Diital, jana Jumatatu Oktoba 2, 2023; Mwakilishi wa Mrajisi wa mkoa huo, Projestus Pascal amesema kuwa jumla ya tani 19,000 zimeuzwa.

“...jumla ya tani 19,000 za mbaazi yenye thamani ya Sh38 billioni zimeuzwa katika minada 11 iliyofanyika sehemu tofauti tofauti mkoani Lindi,” amesema Pascal.

Kwa upande mwingine wakulima wa zao hilo mkoani humo, wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupata bei nzuri.


Ally Mbogo, Mkulima kutoka Kata ya Mkwajuni, Manispaa ya Lindi, amesema changamoto ya ukosefu wa soko, iliwasababishia kuuza zao hilo kwa bei ya chini.


"Mwaka 2020 nililima mbaazi, lakini nilipata hasara, hakukuwa na soko, tulikuwa tunaamua kufanya mboga na ikafikia kipindi nikaacha kulima, nikawa nalima ufuta na korosho, lakini mama Samia alipoamua mfumo wa Stakabadhi Ghalani, kuingia kwenye mbaazi, tunashukuru sana mwaka huu kwakweli tumeuza bei nzuri, licha yakwamba mnada huu wa mwisho bei imeshuka kidogo". Amesema Ally


Nae, Subira Juma mkulima wa mbaazi, amesema kuwa bei inaridhisha kwa sasa tofauti na walivyokuwa wanauza mwanzoni, kwani walikuwa wanalima zao hilo bila ya kupata faida.

Makamu mwenyekiti wa Chama Kikuu Lindi Mwambao Yassin Hashim amesema kuwa wakulima wajitahidi kuhakikisha mbaazi zinakuwa zinakauka vizuri kabla ya kupeleka ghalani kutokana na kuepusha unyevu na kusababisha kupeleka mbaazi ambayo haina ubora.

"Msimu ujao wakulima wa zao la mbaazi wajitahidi kuhakikisha wanapeleka mbaazi zenye ubora, ilikuweza kujakupata bei nzuri zaidi, na niwaombe wakulima wa zao hili la mbaazi walime kwa wingi sana kwa sasa mbaazi ni biashara," amesema Hashim.