Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAENDELEO: Gesi inaweza kuokoa elimu-Lowassa

Muktasari:

  • Inaweza kutumika kuchochea kukua kiwango cha elimu na ajira

Arusha. Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amesema nchi inaweza kutumia rasilimali ya gesi iliyogunduliwa kupunguza kushuka kwa kiwango cha elimu.

Akitoa salamu katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Kati mjini hapa jana, Lowassa alisema utajiri huo wa gesi unaweza kutumika kuinusuru elimu pamoja na vijana kuondokana na tatizo la ajira.

“Mungu ametujalia utajiri wa gesi, nafikiri  mahali sahini kuelekeza fedha za gesi ni  kwenye elimu itakayokuwa bora na kujibu mahitaji ya sasa,” alisema na kuongeza: “Huko vijijini wazazi hawana uwezo, tukitumia fedha hizi tunaweza kuwasaidia watoto wakapata elimu bora na ya kisasa.

“Elimu hii lazima itatue tatizo la ajira na ndiyo maana kila siku nasema elimu inatakiwa iwe kwanza, kilimo baadaye...mtu akipata elimu ndiyo ataweza kuendesha kilimo.”

Lowassa alisema kutanguliza kilimo kabla ya elimu ni matumizi mabaya ya matrekta kwa kuwa yanatumika tofauti na ilivyotarajiwa ikiwamo kubeba maharusi.

“Nilisema Kilimo Kwanza ndiyo, lakini hakiwezi kuwa kwanza kabla ya elimu...tanguliza elimu halafu ndiyo uje na kilimo. Ukitanguliza kilimo, ndiyo watu wanachukua power tiller na kubeba maharusi,” alionya.