Ving’amuzi DSTV vyashushwa bei

Dar es Salaam. Ili kunogesha sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya, Kampuni ya MultiChoice Tanzania imetangaza neema ya burudani kwa wateja wake.
Kuanzia jana (Novemba 17, 2023) hadi Januari 2, 2024 king’amuzi cha DSTV kitakuwa kikiuzwa Sh59,000 kikiambatana na kifurushi cha Shangwe mwezi mmoja bila malipo.
"Tutakuwa na kampeni katika msimu huu yenye lengo la kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanapata huduma hii ili wafurahie burudani, elimu na habari wao na familia zao msimu huu wa sikukuu,” alisema Kaimu Mkuu wa Masoko wa DStv, Semu Bandora.
Alisema wateja wao sasa watapata burudani zaidi za kusisimua kupitia soka, filamu, tamthilia, katuni na vipindi mbalimbali vya watoto vitakavyoileta familia pamoja na kuimarisha upendo.
Kwa upande wa Meneja Maudhui wa Kampuni hiyo, Noel Mulumba alisema katika msimu huu kumeongezwa maudhui kedekede kwa wateja, ikiwemo chaneli ya Sikukuu ya “Holiday Pop Channel DStv 198.”
Akizungumzia msimu wa sikukuu, mteja Neema Mtengwa, mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam alisema: “Binafsi kila tunapofikia kipindi kama hiki cha kuelekea sikukuu huwa nakifurahia kwa sababu sisi wateja tunafaidika sana na mapunguzo mbalimbali ya bidhaa kutoka kampuni tofauti tofauti.
Naye Prosper Andindilile, mkazi wa Keko alitoa pongezi kwa DStv kwa kuja na mpango wao wa kunogesha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.