Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Muktasari:
- Imamu aliyeteka vichwa vya habari mitandaoni siku za hivi karibuni kupitia video fupi iliyosambaa ikimuonyesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.
Dar es Salaam. Imamu aliyeteka vichwa vya habari mitandaoni siku za hivi karibuni kupitia video fupi iliyosambaa ikimuonyesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.
Tukio hilo ambalo liliibua hisia za watu mbalimbali baada ya kumuonesha Imam huyo kutoonyesha kutetereka na kutomfukuza paka huyo wala kukatisha swala hiyo ambayo huswaliwa kila siku usiku katika mwezi mzima wa Ramadhan.
Kwa mujibu wa tovuti ya Breaking latest News Imamu huyo aliyetajwa kwa jina la Walid Mahsas kutoka nchini Algeria ametunukiwa tuzo na Ofisi ya masuala ya dini iliyo chini ya serikali ya nchi hiyo kwa kuonyesha kwake taswira ya kwamba uislamu pia unazingatia huruma na upendo kwa wanyama.