Mahakama yatoa uamuzi ndoa ikivunjika kila mtu kuchukua chake

Muktasari:

  • Mahakama ya Kuu nchini Kenya Ijumaa Januari 27, 2023 ilitoa uamuzi kuwa wanandoa wanaoachana hawatagawana mali nusu kwa nusu (50/50) kama ilivyokuwa awali, bali kila mmoja atatakiwa kuondoka na kilicho kuwa chake kwa kuonyesha vithibitisho halali.

Mahakama  Kuu nchini Kenya Ijumaa Januari 27, 2023 ilitoa uamuzi kuwa wanandoa wanaoachana hawatagawana mali nusu kwa nusu (50/50) kama ilivyokuwa awali, bali kila mmoja atatakiwa kuondoka na kilicho kuwa chake kwa kuonyesha vithibitisho halali.

Awali, kuhusu sheria ya mgawanyo wa mali nusu kwa nusu kwa wanandoa walioachana, iliibua mjadala kuwa ni kandamizi kwa wanaume, ikizingatiwa kwamba wapo baadhi ya wanaume hujijenga mapema kabla ya ndoa kuliko wenza wao.

Jopo la majaji watano lililoongozwa Naibu Jaji Mkuu, Philomema Mwilu walieleza kwamba kila mwanandoa atatakiwa kuthibitisha mchango wake au mali zilizopatikana ili kuiwezesha mahakama kubaini mgawanyo wa mali.

“Uamuzi huu wa mahakama utaleta usawa wa mgawanyo wa mali kwa wanandoa waliotalakiana,” amesema Jaji Mwilu.

Uamuzi huo ni marekebisho ya Ibara ya 45 (3) ya Usawa katika Ndoa. Ukiweka bayana kila mwanandoa atatakiwa kuonesha mchango wake kwenye mali zilizopatikana.

Mahakama imeeleza kwamba kwamba usawa kwenye ndoa haimaamishi 50/50 hata kwenye umiliki wa mali baada ya ndoa hiyo kuvunjika, isipokuwa mgawanyo unapaswa kuangalia mchango binafsi wa kila mtu pindi wanapogawana mali.

Hata hivyo mahakama hiyo ilieleza kwamba mchango wa unaweza ukawa wa moja kwa moja wa fedha au au isiwe moja kwa moja kama vile kulea familia nyumbani au kuwatunza watoto.