Polisi yawatawanya waandamanaji Mathare Kenya

Kenya. Leo Alhamisi Machi 30, 2023 hali ya utulivu imetawala katika maeneo mbalimbali Jiji la Nairobi huku shughuli zingine zikiendelea kama kawaida, ambapo hali hiyo ni tofauti na siku ya Jumatatu ambapo wenye maduka mengi walikuwa wamefunga biashara zao.

LIVE: Maandamano Wakenya washikilia msimamo wa Odinga

Shughuli za mbalimbali za usafiri zimeendelea kama kawaida na hata idadi magari ya usafiri wa umma maarufu ‘Matatu’ yameonekana kuendelea na shughuli zake za kuingia na kutoka maeneo ya mjini.

Jeshi la Polisi nchini humo limeendelea kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali ili kulinda wananchi na mali zao.

Hali ni tofauti na Mathare ambako tayari polisi na waandamanaji wanakabiliana huku picha zinazonyeshwa na vituo vya runinga zikionyesha polisi wakitupa gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.

Tangu Machi 20, 2023 maandamano ya Muungano wa Azimio yakiongozwa na Raila Odinga yamekuwa yakifanyika hasa jijini Nairobi, Kisumu, Siaya na Migori na kaunti ziingine.

Endelea kufuatukua Mwananchi Digital tutakuletea matukio mbalimbali yatakayojiri.