Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa Marekani aanguka jukwaani, Ikulu yatoa tamko

Wasaidizi wa Rais wa Marekani, Joe Biden wakimsaidia baada ya kujikwaa jukwaani. Picha na mtandao.

Muktasari:

  • “Yuko sawa. Kulikuwa na mfuko wa mchanga jukwaani alipokuwa akipeana mikono,” Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ben LaBolt ameandika.

Marekani. Ikulu ya Marekani ‘White House’ imesema Rais Joe Biden yuko sawa baada ya kujikwaa na kuanguka kwenye jukwaani alipokuwa kwenye sherehe za kuhitimu za Chuo cha Jeshi la Wanaanga huko Colorado Marekani.

 Biden alielekeza kitu ambacho kilikuwa kimeshika mguu wake kilichomsababisha aanguke ambacho kinafanana na mfuko mdogo wa mchanga.

Baada ya kuinuka alionekana kuwa vizuri, akitembea bila msaada huku akitabasamu.

Kupitia Shirika la Habari la CNN limetoa taarifa ya Ikulu ya White House isemayo Rais alikuwa sawa baada ya kuanguka na baadaye alitania kuhusu jambo hilo, akisema kwa wanahabari ‘Nimetiwa mchanga!’


Ilivyokuwa

Biden (80) alianza kukimbia, akitoka mahali alipokuwa akitoa hotuba kwa wahitimu wa chuo hicho. Tukio ambalo lilitumia zaidi ya dakika 90 kutoa stashahada na kuwapongeza mamia ya wanafunzi.

Alipokuwa akielekea kwenye kiti chake, alijikwaa na kuanguka chini. Rais alitua kwenye nyonga yake ya kulia kabla ya kuinuka ambapo maafisa wake, ikiwa ni pamoja na afisa wa Chuo cha Jeshi la Anga, walishika mikono ya Biden kumsaidia.

Alipoinuka, Biden alielekeza kwa kutumia vidole vyake kuwa chini kuna kitu kilikuwa kimeshika. Video ya wakati huo ilionyesha mifuko ya mchanga iliyowekwa mbele ya jukwaa karibu na mahali ambapo Biden alikuwa amesimama.

Rais alirudi kwenye kiti chake bila msaada, na alionekana mwenye furaha wakati sherehe inahitimishwa.

“Yuko sawa. Kulikuwa na mfuko wa mchanga jukwaani alipokuwa akipeana mikono,” Mkurugenzi wa Mawasiliano Ben LaBolt aliandika kwenye Twitter.


Imeandaliwa na Sute Kamwelwe.