Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tetemeko la ardhi laua 118, lajeruhi 580

Mwenekano wa eneo lililoathirika na tetemeko. Picha na IndianExpress

Muktasari:

Wakazi waishio kwenye milima kwenye ukingo wa Kaskazini mwa nyanda za juu za Qinghai-Tibet ndiyo walioathirika zaidi na tetemeko lililoua watu 118.


Dar es Salaam. Watu 118 wamefariki dunia huku wengine 580 wakijeruhiwa kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea usiku wa kuamkia leo, Jumanne Desemba 19, 2023 nchini China.

Kwa mujibu wa Reuters, tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.2 katika kipimo cha richa limeipiga eneo la milima kwenye ukingo wa Kaskazini mwa nyanda za juu za Qinghai-Tibet.

Inaelezwa kuwa hali ya uokoaji imekuwa ngumu kutokana na uwepo wa baridi kali katika eneo hilo hivyo majeruhi wanahofiwa kuongezeka.

Kwa mujibu wa Kituo cha Mitandao ya Tetemeko la China (CENC) kimesema pia tetemeko limeathiri kaunti ya Jishishan katika jimbo la Kaskazini Magharibi la China la Gansu.


Hata hivyo, matetemeko ya ardhi ni ya kawaida katika mikoa ya magharibi kama vile Gansu, ambayo iko kwenye mpaka wa Mashariki wa uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet.

Katika miongo ya hivi karibuni nchini China, tetemeko kubwa la ardhi kutokea lilikuwa mwaka 2008 likuwa na ukubwa wa richa 8.0 na liliua takriban watu 70,000.

MWISHO