Tinubu aitaka Niger kurudisha utawala wa kiraia

Rais wa Nigeria, ambaye pia ni mwenyekiti wa Ecowas, Bola Tinubu.

Muktasari:

  • Jeshi la Niger limehitimisha makubaliano ya kijeshi na Benin, huku kukiwa na mgogoro wa kikanda kuhusu kupelekwa, wanajeshi katika nchi hiyo.

Niamey. Rais wa Nigeria, ambaye pia ni mwenyekiti wa Ecowas, Bola Tinubu amependekeza kuwapo na utawala wa mpito wa miezi tisa  ili kuifanya nchi hiyo kurudi kwenye utawala wa kiraia.

 Awali Jeshi la Niger lilitangaza kwamba litashikilia madaraka kwa muda wa miaka mitatu.

Hata hivyo, wanajeshi wa Niger jana Jumanne waliishutumu Seriklai ya Benin kutuma askari wake nchini humo.

Jumuiya ya Ecowas imejaribu kujadiliana na viongozi wa mapinduzi yaliyofanyika Julai 26 nchini Niger, lakini imesema ikiwa juhudi za kidiplomasia zitashindwa iko tayari kutumia nguvu kama suluhu ya mwisho ili kurejesha utulivu.

Taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa ilisema Benin imeamua kutuma wanajeshi pamoja na vifaa vya kivita kuendana na matakwa ya Ecowas.

Jumuiya ya Ecowas ilisema bado ipo kwenye mazungumzo ili kujua hatima ya kupata usuluhishi katika taifa la Niger.


Imeandikwa na Albetina Menas kwa msaada wa mashirika.