Uingereza yaahidi Brexit kabla ya Chrismass

Muktasari:

Ni baada ya chama cha Conservatives kushinda uchaguzi.

London, Uingereza. Waziri wa masuala ya ndani wa chama cha Conservative, Priti Patel amesema kwamba Serikali itahakikisha Uingereza inajitoa katika Umoja wa Ulaya (EU) maarufu Brexit,kabla ya sikukuu za Christmas.

Waziri Patel alisema jana Jumamosi Desemba 14 kuwa kwa sasa hakuna cha kuzuia mpango huo wa Brexit kufanyika haraka kabla ya msimu huo wa msimu huo Christmas.

Naye mbunge wa zamani wa Conservative, Sir Alan Duncan ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Waziri Mkuu, Boris Johnson alisema kiongozi huyo sasa ndiye mwanasiasa mwenye umaarufu mkubwa Uingereza na kwamba uchaguzi huo umethibitisha hilo.

Mbunge huyo aliliambia Shirika la Utangazaji la BBC kuwa ‘’sasa tutaweza kutawala kwa wingi wa kura.”

Awali mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Labour, Ian Lavery ambaye ameweza kutetea kiti chake cha ubunge alisema kwamba Waingereza walifanya uamuzi kulingana na matakwa yao.

Naye John McDonald ambaye ni mbunge kutoka kambi ya upinzani alisema kwamba matokeo hayo ya uchaguzi yamemsikitisha.

‘’Nilidhania ushindani utakuwa wa karibu mno’ lakini hali imekuwa tofauti,” alisisitiza mbunge huyo.

Hata hivyo, mbunge huyo alisema Conservative hawakuwatendea haki wanachi kutokana na kutumia uchaguzi huo kama ni wa masala ya Brexit pekee wakati Waingereza walitarajia kusikia mambo mbalimbali.

“Wananchi walikuwa wakisubiri mambo mengine yachipuke na si kuhusu Brexit pekee, hatukuwatendea haki kabisa,” alisema mbunge huyo.