Fursa za kibiashara katika mpira wa miguu

Wakati mimi na wewe tunaishia kubishana kuhusu mpira wa miguu kwa sababu ya tofauti zetu za kishabiki, hatunufaiki chochote.
Nyakati hizi mpira wa miguu siyo tu burudani bali ni zaidi ya biashara kuanzia kwa mchezaji mwenyewe, kocha na mtu yeyote asiye mchezaji.
Kwa kuwa mpira wa miguu ndiyo mchezo unaopendwa zaidi duniani na kusababisha vijana wengi nchini na nje ya nchi kujiingiza katika ushabiki, watu mbalimbali wenye jicho la mbali katika biashara hawajaacha kutumia fursa za kibiashara zilizopo katika mpira.
Kuna fursa kadhaa za kujiajiri kupitia soka ikiwa vijana watazielewa badala ya kupoteza muda mwingi pasipo manufaa kiuchumi.
Mpira wa miguu ndiyo mchezo pekee ambao huingiza kipato kikubwa sana katika mataifa mbalimbali kama Uingereza, Uhispania, Misri, Afrika Kusini na Tanzania.
Mpira ni biashara kwa sababu watu wengi wamejiajiri kupitia mpira wa miguu na wanapata pesa nyingi.
Kuna watu wamejikita kufanya uchambuzi na utangazaji wa mpira tu kama Shaffih Dauda, Edo Kumwembe, Kashasha na wengineo.
Kwa hiyo, usiishie kubishana bure pasipo kunufaika chochote, badala yake angalia namna gani unaweza kunufaika kiuchumi katika ushabiki wako.
Baada ya kuona mpira ni pesa, zimeanzishwa kampuni mbalimbali za kutengeneza pesa kupitia mpira, kama kampuni ya michezo ya kubahatisha, kwa mfano; sokabet, sport pesa, m-bet, moja bet na nyinginezo.
Pia, wale wenye jicho la mbali katika kuona fursa za kibiashara katika mpira wa miguu, kuna kampuni mbalimbali zimejikita kutengeneza vifaa vya michezo kama Adidas na Nike.
Hizi kampuni ni maarufu katika utengenezaji wa jezi, soksi na viatu vya michezo.
Tanzania ndiyo kwanza inakua katika soka, je tutaendelea kusubiri Adidas na Nike waendelee kuteletea vifaa au na sisi tutengeneze wenyewe na tuwauzie wachezaji wetu?
Kwa elimu, mafunzo na ushauri usikose kutembelea kurasa zetu Facebook, Instagram na Twitter kwa jina la Elimika Ung’are au piga namba 0766656758/0655056758.