‘Ilikuwa lazima kumuua aliyeshambulia polisi’

‘Ilikuwa lazima kumuua aliyeshambulia polisi’

Muktasari:

  • Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kueleza kuwa hakukuwa na namna ila kumuua mtu aliyewashambulia polisi kwa risasi juzi, baadhi ya wataalamu wa masuala ya usalama wameunga mkono kauli hiyo wakisema kumuua kilikuwa kitendo cha lazima kwa kuwa haikujulikana uwezo na silaha alizokuwa nazo.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kueleza kuwa hakukuwa na namna ila kumuua mtu aliyewashambulia polisi kwa risasi juzi, baadhi ya wataalamu wa masuala ya usalama wameunga mkono kauli hiyo wakisema kumuua kilikuwa kitendo cha lazima kwa kuwa haikujulikana uwezo na silaha alizokuwa nazo.

“Kwa kuwa hakuwa na dalili ya kujisalimisha, hapakuwa na jinsi zaidi ya kumuua. Ingekuwa amewateka na kuwashikilia watu ingekuwa tofauti na kilichofanyika,” alisema Martin Elia, mdau wa masuala ya usalama mkoani Iringa.

Iwapo kungekuwa na vifaa vya kisasa kukabiliana na uhalifu mfano roboti, alisema angeweza kudhibitiwa bila kutumia risasi za moto.

Kilichoendelea usiku huu nyumbani kwa jamaa aliyeua askari wanne

“Hakuna aliyetarajia kungetokea tukio kama lile na muda huo ulikuwa ni wa foleni ndefu barabarani ndio maana askari walichelewa kufika eneo la tukio,” alisema.

Mdau mwingine wa usalama, Benito Frank alisema: “Kwa namna ilivyotokea inaleta maswali mengi kuhusu hali ya ulinzi wetu, lakini ni lazima tuelewe kuwa lilitokea kwa kushtukiza.” Makalla amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kudhibiti tukio hilo alilosema lilizua taharuki.

Wafanyakazi wa Hamza mgodini wamzungumzia

‘‘Wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida. Kama mtu yule aliua watu wanne angeweza kuwadhuru wengi zaidi,” alisema.