‘Mnaotaka uongozi CCM mwaka 2022 shirikini vikao vya shina’

Friday July 09 2021
New Content Item (1)
By Stephano Simbeye

Songwe. Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania wanaotarajia kuwania uongozi utakaofanyika mwaka 2022 watapimwa kwa ushiriki wao katika  vikao vya shina.

Amesema hayo leo Ijumaa Julai 9, 2021 mkoani Songwe katika ziara yake ya siku mbili  akibainisha kuwa wanachama wengi wamekuwa wakidharau vikao vya shina vinavyosimamiwa na balozi wakisahau kuwa ndio msingi na uhai wa chama.

"Kama umejipima unatarajia kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi ndani ya chama mwakani hakikisha unakuwa na muhtasari wa jinsi ulivyohudhuria vikao vya balozi ambavyo ni vikubwa kuliko..., hata mimi napaswa kushiriki vikao hivyo kwenye eneo ninaloishi," amesema.

Chongolo ametua nafasi hiyo kuwaonya watu wanaendekeza fitina zinazotokana na wao kushindwa katika uchaguzi uliopita wa madiwani, wabunge na rais akiwataka wawape nafasi walioshinda watekeleze waliyoyaahidi kwa wananchi.


Advertisement