Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yanena kuhusu Abdul Nondo

Muktasari:

  • Ole Nasha amesema kwa kuwa Nondo ana kesi kama akishinda anarejea chuoni.

Dodoma. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Abdul Nondo amesimamishwa masomo ili kulindwa, asipoteza sifa za kuwa mwanafunzi wa chuo hicho.

Kusimamishwa chuo kwa Nondo, kuliibua mjadala mkali wakati wa kuijadili bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakidai hatua hiyo ni aibu kwa chuo hicho.

Akijibu hoja hiyo leo Mei 2, 2018 bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa wizara hiyo, William Ole Nasha amesema kwa kuwa Nondo ana kesi kama akishinda anarejea chuoni na sheria inamlinda badala ya kumminya asipoteze sifa.