71,000 kufanya mtihani darasa la nne Chunya

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Wanafunzi zaidi  ya 71000 wa darasa la nne wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne katika halmshauri ya Wilaya ya Chunya ambao unaotarajia kufanyika kwa siku mbili october 25 na 26.

Chunya. Wanafunzi 71, 000 kutoka mbalimbali wilayani Chunya, wanatarajia kufanya mtihani wa darasa la nne utakaoanza Oktoba 25 mwaka, na ambao unaotarajia kufanyika siku mbili, huku wasimamizi wakitakiwa kufuata kanuni na taratibu.

 Haya yalielezwa na Ofisa Elimu ya Msingi Fred Mhanze wilayani humo, wakati akizungumza na mwandishi kuhusiana na maandalizi ya mtihani huo ambapo amesema maandalizi yako vizuri na kwamba wanategemea kuongeza ufaulu.

Mhanze amesema kutokana na kufanya vizuri katika mtihani wa mock ya mkoa wanaamini kila mwanafunzi atafanya vizuri na kupata alama za juu.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kiwanja, Yohana Mwakalinga, amesema wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani katika shule yake wamejiandaa vyema kutokana na mitihani ya kujipima walikuwa wakiwapatia kila wiki.

“Tulikuwa tunawaandaa kwa mitihani ya majaribio ya kila wiki, pia katika mtihani wa mock mkoa, shuke yetu kwenye kata ilishika nafasi ya nne hivyo anaamini wanafunzi watafanya vizuri,” amesma Mwalimu huyo.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mayeka Mayeka akizungumzia kuhusu ulinzi na usalama, amesema wapejipanga vizuri na kuwaelekeza wasimamizi wa mitihani kuhusu kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepuka kuvuruga mitihani.

Amesema wasimamizi wamepewa semina hivyo wanatambua majukumu, na kwamba wao kama wasimamizi ulinzi na usalama watahakikisha ulinzi unaimarika.