ADC wafungua pazia fomu za uspika, mmoja achukua

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Siku moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufunga pazia la kuchukua na kurejesha fomu za kuomba uteuzi wa kugombea nafasi ya Spika wa Bunge, Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) nacho kimefungua mchakato huo huku mwanachama mmoja akichugua fomu.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufunga pazia la kuchukua na kurejesha fomu za kuomba uteuzi wa kugombea nafasi ya Spika wa Bunge, Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) nacho kimefungua mchakato huo huku mwanachama mmoja akichugua fomu.

Mwanachama huyo wa ADC, Maimuna Kassim amekuwa wa kwanza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa nafasi ya uspika.

Maimuna mwenye shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa na utawala wa umma amechukua fomu leo Jumapili Januari 16, 2022 katika ofisi za makao makuu ya chama hicho yaliyoko Buguruni jijini Dar es Salaam.

Mwanachama huyo wa ADC amewahi kugombea ubunge katika jimbo la Kilindi mkoani Pwani katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Maimuna amekabidhiwa fomu hiyo na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Doni Mnyamani ambapo gharama za fomu hiyo ni Sh100, 000.

Jana Jumamosi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilihitimisha uchukuaji na urejeshaji fomu ambapo kati ya wanachama 71 waliochukua fomu hizo, 70 walifanikiwa kurejesha huku mmoja akishindwa kurudisha.