Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aga Khan wazindua utoaji huduma za afya Zanzibar

Mariam Mwinyi, Mke wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi akiwa na na Binti Mtukufu, Zahra Aga Khan wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Hospitali ya Aga Khan Polyclinic Mjini Unguja Zanzibar.

Muktasari:

  • Uwekezaji huo uliohusisha kuboresha jengo la hospitali hiyo na kununua vifaa vya matibabu umefanyika kupitia mkopo wa Sh2 bilioni kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

Unguja. Ili kurahisha utoaji na upatikanaji wa huduma za afya Zanzibar, Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) chini ya Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan Tanzania (AKHS) imezindua hospitali (Polyclinic) Unguja.

 Hospitali hiyo ambayo ipo maeneo ya Stone Town, itatoa huduma za macho, kusafisha damu, ukaguzi wa mwili huduma za meno, maabara na dharura.

Uwekezaji huo wa kuboresha jengo la hospitali hiyo na kununua vifaa vya matibabu umefanyika kupitia mkopo wa Sh2 bilioni kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) ambapo kwa mwaka inategemea kuhudumia wagonjwa 150,000 kwa mwaka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hospitali hiyo leo Aprili 25, 2023, Mke wa Rais wa Zanzibar Mariam Mwinyi amempongeza Mtukufu Aga Khan na AKDN kujitolea kwao kuimarisha afya na ustawi wa wananchi duniani kote hususani Zanzibar.

“Serikali inafanya jitihada kubwa kupanua uwezo na ubora wa vituo vya afya na kuboresha afya ya wananchi wake, kipaumbele hasa ni kuboresha utoaji huduma za uzazi, mama mtoto na kijana.

“Tunatambua na kuthamini uhusiano wa Serikali ya Zanzibar na mtandao wa Aga Khan ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 100 kwani AKDN imekuwa ikichangia katika kupunguza umaskini, elimu, afya na maendeleo ya kiuchumi," amesema

Amesema kufunguliwa kwa Aga Khan Polyclinic ni uwekezaji muhimu wa miundombinu ya afya ambao pia itasaidia wataalamu wengine kutoka hospitali za Zanzibar kupata ujuzi huo kupitia hospitali hiyo.

Ameomba AKDN kuangalia namna ya kuwekeza pia na Pemba katika huduma ngazi za msingi huku akimkaribisha Mtukufu Aga Khan pia kuwekeza katika maeneo mengine ya kiuchumi, urithi na amzingira.

Naye Binti Mtukufu,  Zahra Aga Khan amesema tangu walipoanza kutoa huduma za afya mwaka 1929 mpaka sasa AKHS inaendelea kutoa huduma bora, endelevu na za viwango vya hali ya juu.

Alisema kwa mwaka 2021 AKHS ilihudumia wagonjwa zaidi ya milioni moja kwa viwango vya kimataifa hivyo itaendela kuhaikisha hudma bora zinatolewa kwa jamii.

Naye Mkurugenzi wa Tiba na Afya katika taasisi ya Afya ya Aga Khan Tanzania Harrison Chuwa amesema kuna vituo 26 Tanzania nzima na hicho ni cha 27 lakini kwa Zanzibar imepewa kipaumbele kwa kufungiwa vifaa vyote muhimu ikiwemo CT Scan.

Naye Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Nabil Hajlaoui alisema wataendelea kuunga jitihada mkono za marais hao kutokana mipango yao ya kuotoa vipaumbele vyao kwenye elimu na afya kudumisha urafiki huo uliodumu kwa miaka mingi.