Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aga Khan yawezesha walimu mafunzo kwa vitendo

Muktasari:

  • Ili kuwawezesha walimu kuwa na mbinu za mafunzo kwa vitendo, Chuo Kikuu cha Aga Khan kim,etoa mafunzo ya mtalaa unaozingatia umahiri kwa baadhi ya walimu Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Katika jitihada za kusaidia utekelezaji wa mtalaa unaozingatia umahiri (CBC) shuleni, Chuo Kikuu cha Aga Khan kupitia Taasisi ya Maendeleo ya Elimu, Afrika Mashariki (AKU-IED, EA) kimetoa mafunzo ya umahiri kwa baadhi ya walimu.

CBC iliyoanzishwa ili kuhamisha kujifunza kwa kukariri hadi kwa vitendo imelenga kukuza uelewa wa walimu katika ufundishaji.

Kwa kuzingatia mabadiliko hayo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitambua umuhimu wa kuimarisha ujuzi wa walimu, ikilenga kuinua matokeo ya elimu kwa wanafunzi kote nchini.

Chuo Kikuu cha Aga Khan, kupitia Taasisi yake ya Maendeleo ya elimu, kimeendesha warsha ya maendeleo ya walimu kwa miaka 15 sasa, lengo likiwa ni kuunda programu zinazozingatia mahitaji ambazo zina matokeo chanya kwa walimu, kazi zao na jamii.

Akizungumza mwishoni mwa wiki Oktoba 6 katika warsha hiyo iliyofanyika jijini hapa, Mkuu wa AKU-IED, EA, Profesa Jane Rarieya, amesisitiza umuhimu wa program hiyo.

“Programu tuliyotoa leo yenye mada ya ‘ujifunzaji hai’ (active learning) imelenga kukuza uwezo wa wanafunzi," amesema.

Hata hivyo, amesema bado waelimishaji wanakabiliwa na changamoto ya kuelewa mtaala huo.

"Bado idadi kubwa ya walimu hawaelewi kujifunza kwa vitendo, wengi wanafahamu nadharia tu. Ndiyo maana tumeleta warsha hii ili kuwaimarisha mafunzo kwa vitendo wakati wakiwa darasani," amesema Profesa Rarieya.

Amesema warsha hiyo imelenga kuwapa mikakati ya kujifunza walimu hao na kukuza ujuzi na kutathmini uelewa wa wanafunzi.

"Katika warsha nzima, tulikuwa tukionyesha mikakati ya kujifunza, tukiwaonyesha ni ujuzi gani wanaweza kukuza, na pia jinsi unavyoweza kutumika.

"Walimu wanapaswa kuwa na ujuzi, sawa na wataalamu wengine," Profesa Rarieya.

Akizungumzia mafunzo hayo, Mwalimu kutoka shule ya msingi ya Aga Khan, Muyenga Kasongo, yamewasaidia.

“Mwalimu anatakiwa kujifunza kila siku, kila mara kwa sababu dunia inabadilika sana na elimu nayo inabadilika, mafunzo hayo yakipatikana kwa wingi yatatusaidia sana," amesema.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Resing English Medium, Micah Wilson, ameunga mkono kauli hiyo akisema, “Kama mwalimu, unapaswa kujifunza kitu kipya kila wakati kwa sababu dunia inabadilika. Warsha ya namna hii inatupa maarifa mapya na tumeweza kujifunza mbinu na njia nyingine za kufundisha kwa weledi tukiwa darasani."

Mtaalamu wa elimu, Dk Thomas Jabir amesema program hiyo ina lengo la kuziba pengo kati ya mbinu za ufundishaji asilia na matakwa ya CBC.