Ajali za pikipiki bado tishio kwa Tanzania, Afrika

Uzinduzi wa kampeni ya Mpango wa Safiri Salama na Usalama wetu kwanza ya mkoani Njombe Mei 28, 2021. Katika tukio hilo, elimu ilitolewa kwa madereva wa pikipiki na bajaji.

Muktasari:

  • Matukio ya ajali za barabarani yanashika nafasi ya nane duniani kwa kusa­babisha vifo.

Matukio ya ajali za barabarani yanashika nafasi ya nane duniani kwa kusa­babisha vifo.Na hii kwa kiasi kikubwa inasababishwa na namna matukio hayo yanavyotokea kwa kuogofya mara kwa mara, siku baada ya siku, pengine hata saa baada ya saa.

Pia takwimu zinaonye­sha kuwa asilimia 40 ya waathirika wa ajali za barabarani ni watembea kwa miguu nchini huku asil­imia 60 ikibakia kwa watu­miaji wengine wa barabara kama vile waendesha boda­boda, baiskeli na magari.

Kinachostaaajibisha wen­gi kwa miaka ya hivi karibuni matukio ya ajali zitokanazo na pikipiki (maarufu kama ‘bodaboda’) ni mengi zaidi kuliko yale yatokanayo na vyombo vingine vya moto.

Biashara ya pikipiki ni moja ya sekta muhimu za usafiri nchini ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kupunguza changamoto ya foleni nyakati ambazo tuta­hitaji kufika katika maeneo ya kazi, shule, hospitali, michezoni nk.

Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa akiwa katika moja ya vikao na wadau wa usafirishaji na usalama barabarani.

Ni usafiri rahisi na pend­wa miongoni mwa watu wengi kwa uwezo wake wa kuwafikisha kule wanakoele­kea kwa haraka zaidi licha ya miaka ya karibuni kuoneka­na kuwa si salama kulingana na mambo mbalimbali.

Barabara zimekuwa machinjio ya waendesha bodaboda wasio makini na hata wale wanaojitahidi kumakinika. Na hili lina­ufanya usafiri huo ulioajiri idadi kubwa ya Watanzania wa kipato cha chini kuwa si salama zaidi.

Kulingana na tafiti, wanau­me ni wahanga wakubwa wa matukio ya ajali za boda­boda kwa kuwa hulazimika kutumia muda mwingi na nje ya masaa ya kawaida ya kazi, kutafuta riziki zao wakiwa barabarani baada ya kuhakikisha wameshakamil­isha mahesabu ya mmiliki wa chombo.

Tatizo hilo si tu limekuwa janga la Taifa bali limeende­lea kuwa tishio na kuathiri nchi nyingine za ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Moja ya sababu za ajali ni tabia ya baadhi ya madereva pikipiki hao kutokufuata matumizi sahihi ya baraba­ra na sheria zinazoongoza usalama barabarani kuwa moja ya sababu  hatarishi za ajali hizo.

Uzinduzi wa kampeni ya Mpango wa Safiri Salama na Usalama wetu kwanza ya mkoani Njombe Mei 28, 2021. Katika tukio hilo, elimu ilitolewa kwa madereva wa pikipiki na bajaji.

Kwa tafsiri rahisi, kutoku­fuatwa kwa sheria hizo za usalama barabarani kuna­husisha kutokuvaa kofia ngumu (helmet) kwa made­reva wengi, tabia ya kupa­kia abiria zaidi ya mmoja (mishikaki), matumizi ya vileo, kutokupitia mafunzo rasmi ya uendeshaji pikipiki nk.Zipo sababu nyingine ambazo hazipewi nafasi kubwa lakini ni miongoni mwa vyanzo vya ajali za pikipiki.

Suala la miundom­binu kwa baadhi ya maeKariakoo eneo ambalo lime­banana kiasi cha watumia barabara kukosa nafasi ya kupita na kusababisha ajali wakati mwingine.

Mitazamo ya visababishi vya ajali za pikipiki hata kwa madereva bodaboda imega­wanyika miongoni mwao. Wapo wanaokubali huwa zinatokana na uzembe wao na wanaosema kuwa huwa wanasababishiwa.

Mwenyekiti Mstaafu wa Kituo cha Bodaboda cha Mwananchi, Rashid Mwan­ga ambaye ana uzoefu wa miaka 10 ya biashara ya pikipiki yeye anaamini kuwa ajali hutokana na mambo yote mawili, uzembe na wakati mwingine kusa­babishiwa.

Akielezea matukio ya ajali aliyoyapata na hatakaa kuyasahau, ambayo baadhi ni ya kujitakia na mengine ya kusababishiwa, anaikum­buka kwa karibu zaidi ajali aliyoipata maeneo ya Taba­ta Bima.“Unajua ukiwa baraba­rani huku umetawaliwa na mawazo mengi basi unaweza ukajisahau.

Nili­kuwa nimepakia abiria wan­gu mmoja naelekea naye Segerea, wakati nakarib­ia njia pacha ya kwenda Kimanga na Segerea nikiwa katika mwendokasi niliji­kuta nahamasika kulivuka gari ambalo lilishanionye­sha kuwa linakuja uelekeo wangu hivyo nikaligonga na kuanguka chini.

Kwa kuwa nilikuwa nimevaa kofia ngu­mu niliteleza kwa kichwa mpaka mtaroni.”Mwanga anakiri kuwa sehemu kubwa ya ajali hiyo anaona ni uzembe wake na alichubuka kidogo mwilini.

“Kitu kingine nachomshu­kuru Mungu abiria wangu yule alifanikiwa kuruka mapema alivyoona kuwa chombo kinapoteza uele­keo.”

Anasema pia alishawahi kupata ajali maeneo ya Taz­ara wakati daraja la juu la Mfugale likiwa katika hatua za mwisho za ukamilikaji.

Mwanga anaongeza zaidi kuwa watu wa daladala nao kwa asilimia kubwa wanachangia kuwapo kwa ajali za pikipiki nchini.

Katika mahojiano hayo anaeleza sababu zinazo­changia kuongezeka kwa ajali za pikipiki ikiwamo; umakini mdogo miongoni mwa waendesha bodaboda, kutokuzingatia kanuni za usalama barabarani, elimu ndogo miongoni mwa waendesha bodaboda nk.

Naye Katibu wa Kituo cha Bodaboda cha Mwanan­chi, Mwita Magele anas­ema ana uzoefu wa miaka 7 katika biashara hiyo na anakiri kuwahi kupata ajali japo ni zile ndogo ndogo na anadhani kuwa ajali zitaendelea kuwepo kwa sababu ya kundi dogo miongoni mwa waendesha bodaboda kutokutaka kutii sheria na kanuni za usala­ma barabarani.

“Unajua sisi bodaboda tunaonekana wahuni na tunadharaulika kutokana mienendo na tabia zetu na hii ndiyo sababu wakati mwingine ya kupata ajali za mara kwa mara,” anaeleza zaidi.

Katika upande mwingine, Magele anaamini kuwa hata maofisa wa usalama baraba­rani wakati mwingine nao ni chanzo cha ajali kwa kuwa baadhi ya waendesha boda­boda wanaohisi kuwa na makosa kujaribu kuwakwe­pa maofisa hao na kwa saba­bu matukio hayo hufanywa katika mazingira hatarishi zaidi, inasababisha ajali kutokea.

Magele, katika nafasi yake ya ukatibu ambayo ameihudumu mara mbili katika vipindi viwili tofauti, anasema, “sisi katika kituo chetu cha Mwananchi huwa tunamuomba Mungu sana na kwa kweli kumekuwapo na majanga madogo mado­go na katika miaka saba ya uongozi hatujawahi kupata tukio la ajali lililosababisha kifo ispokuwa kuvunjika kwa mguu kwa mwenzetu mmoja,” anaeleza.

Taasisi ya Tiba za Mifupa ya Muhimbili (MOI) ime­kuwa ikipokea majeruhi si chini ya 10 mpaka 15 kwa siku wa ajali zinazohusisha pikipiki.Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kufikia hadi majeruhi 20 kwa siku kunapokuwepo kwa matukio rasmi makubwa ya kiserikali yanayokusanya idadi kubwa ya watu, mpira nk.

Kulingana na uzoefu, ajali hizo zimekuwa zikisababi­sha majeraha kwa zaidi ya mtu mmoja (kwa maana dereva, abiria na mtu wa tatu kutoka katika chombo kingine kilichohusika na ajali).

“Wengi wanapata majeraha ya aina mbalim­bali yanayohusisha miguu, kiuno, kichwa, kifua wakati mwingine na inategemea ajali hiyo imetokana na nini; wakati mwingine ni pikipiki kwa pikikipi zinagongana, wakati mwingine pikipiki kwa gari na pia, pikipiki kwa waenda kwa miguu,” anaele­za Dk Kennedy Nchimbi kutoka Taasisi ya Tiba za Mifupa Muhimbili (MOI).

Pia, anasema kuwa wengi wao hupata majeraha ya kuvunjika mfupa wa mguu ambao unakuwa na kidonda.

Majeruhi wengi hufiki­shwa kwa dharura, wapo wale ambao wanashindwa kupatiwa matibabu katika mikoa yao husika na kupele­kwa MOI na wengine hut­ibiwa na hospitali zingine za serikali za rufaa kama vile Hospitali ya Temeke, Mwa­nanyamala na Amana.

Hali hiyo inasababisha kuwe na mlundikano wa wagonjwa ukizingatia wen­gi wao hupata majeraha makubwa ambayo matibabu yake pengine yanahitaji siku nyingi kuweza kuwarudisha katika hali zao za kawaida.

Akijibu swali kuhusiana na uwezekano wa majeraha hao kupata maambukizi kutokana na vidonda baada ya ajali, Dk Nchimbi anas­ema ajali inatokea baraba­rani na kwa mfano mtu anagongwa halafu anatum­bukia katika mtaro wa maji machafu (yawe ya mvua au yale yanayohusisha vyoo) na mkono wake uliopata jeraha ukagusa maji hayo, inaweza kusababisha jeraha kuwa kubwa zaidi na hata mtu huyo kupoteza mfupa wa mkono.

Majeraha mengine yanayoweza kumpata mtu ni katika kiuno kumbuka unapokuwa katika boda­boda unakuwa umekaa umetanua miguu, na mko watatu hadi wanne, unawe­za ukapata jeraha baya zaidi la kupoteza kikombe cha kiuno inapotokea ajali kwa sababu mwendo wa pikipiki na mwendo wako unaku­wa sawa wakati pikipiki inatembea.

Kwa mtu aliyepata jera­ha la kuvunjika kiuno hata kama atatibiwa bado yuko katika hatari ya kupata ulemavu wa kudumu kama vile kushindwa kufanya shughuli zingine za kimwili kama vile kushiriki tendo la ndoa, kushindwa kutembea kama hapo awali.

Wapo ambao wanapata ajali na kupata maambukizi kutoka eneo alilopatia ajali kupitia kidonda mguuni na baadaye mguu huo kuathiri­ka kiasi cha kutaka kuoza na hivyo taratibu za kuukata mguu zitachukuliwa.

Inawezekana pia wakati mwingine mtu anapata maambukizi ya vijidudu ambavyo vinakwenda kati­ka damu na kuathiri eneo fulani ambalo litashindwa kufanya kazi kwa baadaye na kupoteza moja kwa moja kiungo hiko.

Kutokuvaa kofia ngu­mu maana yake unatu­mia kichwa kama ngao, na ipotokea umerushwa na kwenda kugonga eneo fulani utapata maumivu ya kichwa yatakayosababisha damu kuganda kichwani na mwishowe kupata changa­moto ya uzezeta.

Kwa jicho lingine, ajali za barabarani zina athari kub­wa za kijamii na kiuchumi. Kulingana na Dk Kiwango, miongoni mwa athari hizo ni upotevu wa mali, uharibifu wa miundombinu, kupun­gua kwa nguvukazi katika uzalishaji mali, ulemavu wa kudumu, nk.Katika miaka michache iliyopita, Serikali na wadau wake wengine wamekuwa macho katika eneo hili la ajali za barabarani.

Jambo ambalo limesa­babisha leo kuwapo kwa jitihada mbalimbali za kud­hibiti biashara ya usafiri wa bodaboda ili kupunguza ajali; ikiwamo mafunzo kwa waendesha bodaboda husu­san kwa wale ambao hawak­upata mafunzo rasmi.Sambamba na jitihada, pia Serikali iliweka katazo la uuzwaji wa pombe za kati­ka vifungashio vya plastiki (viroba) ambazo zilikuwa zikitumiwa aghalabu na waendesha bodaboda wengi na kuhatarisha usalama wa abiria, na wakati mwingine kusababisha ajali.

Kampeni ya kudhibiti matumizi ya pombe ili­yofanyika wilayani Moshi chini ya Dk Kiwango, Mkoa wa Kilimanjaro ni moja ya mikakati hiyo.

Pia, ipo mika­kati ya uboreshaji wa mifu­mo ya ukusanyaji wa taarifa za ajali za pikipiki.MOI nayo kupitia wawakil­ishi wake wa afya wameku­wa wakipitia vituo vya bod­aboda na kutoa elimu kwa kundi hilo.

Anaeleza kuwa wameshafanya hayo kati­ka maeneo ya Kinondoni, Ubungo na Magomeni laki­ni pia wamekuwa wakitoa elimu mahususi kwa wag­onjwa wenyewe kwa kuwa wao ndiyo walengwa namba moja licha ya wagonjwa wengi kutokusikiliza elimu hiyo kutokana na kuugulia maumivu ya majeraha wali­yoyapata.

Majeruhi kutoka MOI na sehemu zingine huelezwa athari ya kutokuz­ingatia sheria za usalama barabarani na kuwashauri nini wanatakiwa kufanya baada ya matibabu yao.

Magele anathibitisha kuwa kituo chao ni moja ya vituo bora na vya mfano kwa kuwa asilimia kubwa ya wanachama wana mafunzo muhimu ya usalama baraba­rani kwani kupitia viongozi wa mkoa wa waendesha bodaboda waliweza kuomba mafunzo hayo kutoka kwa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani.

Hivyo anasema fursa za mafunzo zipo lukuki huku akitolea mfano wa Chuo cha Ufun­di cha Polisi, Kurasini pia kuendesha mafunzo ya aina hiyo kwa wanaohitaji.

“Hapa katika kituo chetu, asilimia kubwa ya waendesha boda­boda wanamiliki vyeti vya kuhitimu mafunzo.”Kama hiyo haitoshi, na kwa kuwa tatizo hili linahi­taji nguvu ya pamoja, Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani limeendesha programu za mafunzo kwa zaidi ya madereva 500 na kupatiwa vyeti wilayani Makambako, Njombe.

Pia, limefanya kwa Mkoa wa Mbeya kwa kuwafundisha madereva zaidi ya 300.Hatua hizo miongoni mwa nyingine nyingi zimezaa matunda kwani idadi ya matukio ya ajali zitokanazo na pikipiki zimepungua.

Idadi ya majeruhi wawili wa ajali za pikipiki waliokuwa wakifikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku mwaka 2015-16 imepungua na hatimaye kufikia maje­ruhi mmoja kwa siku hos­pitalini hapo mwaka 2019.

Bado kuna imani kubwa kuwa idadi hiyo itaendelea kushuka.Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani inayo mezani mikakati mitatu kabambe ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabrani hususan za pikipiki.

Kaman­da wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa anasema mkakati wa kwan­za mkubwa ni zoezi la kue­ndelea kutoa elimu kupitia madawati ya elimu.

Mkakati wa pili ni ushauri endelevu kwa waendeshabodaboda kwa kuwaambia nini wanapaswa kukifanya wanapohitimu mafunzo kwa maana ya faida na hasara za kutokufuata sheria za usala­ma barabaani.

Mkakati wa tatu na wa mwisho, anasema ni kusi­mamia sheria zenyewe.

Na tayari Jeshi hilo linaendelea na operesheni mbalimbali nchini ya kukamata pikipiki zinazokiuka utaratibu na kuzifungulia mashtaka na kisha kuzipeleka mahaka­mani.

Kamanda anafafanua kuwa kasumba iliyojen­geka miongoni mwa watu wengi kuwa madereva wa vyombo vingine vya moto huweza kubadili mienendo wanapokabidhiwa pikipiki si kweli kwani kama dereva anatii sheria za usalama barabarani bado ataendelea kufanya hivyo bila ya kujali ni chombo gani anakitumia kwa wakati huo.

Anasema hao ambao wanaamini hivyo ni kati ya wale madereva wachache wakaidi na hawa­na nia njema.

Kulingana na utafiti ulio­fanywa, kuna maeneo mengi ambayo kama nchi tunaweza kuboresha ikiwamo kuanga­lia namna ya kudhibiti tabia hatarishi za waendesha bodaboda wengi kuendesha kwa kutozingatia usalama, ulevi wakati wa kuendesha na suala la mikataba na waa­jiri wao ambalo linawalaz­imu kutumia muda mrefu kufikisha hesabu za mwajiri na zake binafsi.

Kuna fursa ya kuboresha huduma kwa majeruhi wa ajali za pikipiki baada ya kutokea kwa ajali, ukusan­yaji wa taarifa zao na ujen­gaji uwezo kwa huduma za kwanza kwa majeruhi hao katika ngazi ya jamii.

Ili kukabiliana na ajali za pikipiki, bado kuna umuhimu wa kuendeleza tafiti hizo ili kutambua, kuboresha na kudhibiti michakato yetu kwa wakati wote.

Pia, kwa upande wa Seri­kali, wadau wanaeleza uhi­taji wa kuwapo kwa sera na mifumo ambayo itasaidia kuweka mfumo utakao­saidia waendesha bodaboda kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa na usalama zaidi.

Mwenyekiti wa Waende­sha Bajaji Kituo cha Mwa­nanchi, ambaye kabla ya kuhamia katika biashara hiyo ya sasa aliwahi kuen­desha bodaboda, Japhet Kamuga anaufananisha mfumo wa uendeshaji biashara ya usafiri wa bod­aboda kama ulivyo ule wa elimu hapa nchini.

Kamuga ambaye ana uzoefu wa miaka 10 wa biashara ya bodaboda anas­ema tangu usafiri huo uingie hapa nchini hakukuwapo na mfumo mzuri wa kuusi­mamia na ndiyo sababu ajali nyingi zinatokana na usafiri huo kwa sasa.

“Tulioupokea ghafla, tukaishi nao na ndiyo maana sasa unatutesa kwa sababu ya kutokuwekea misingi imara.”Anasema kuwa leo hii ukimchukua dereva mwe­nye leseni C kutoka NIT ambaye anafuata sheria zote za usalama baraba­rani na ukaamua kumpa pikipiki aendeshe, unaweza ukashangaa anavyobadilika ghafla kwa kuwa dereva asi­yetii sheria wala kanuni za usalama barabarani ndani ya muda mfupi.

Anaendelea kusisitiza kuwa kwa bahati mbaya biashara hii wakati inaingia hapa nchini vijana wengi ambao hawakuwa na ajira ndiyo walioikimbilia akibainisha kuwa ni zaidi ya asilimia 80 ya kundi hilo.

“Kwa hiyo mimi niseme hili janga limeikumba nchi yetu tayari ambapo hata elimu itolewe kwa kiasi gani lakini bado madereva boda­boda wataendelea kubakia na mienendo yao ile ile ya siku zote,” anahitimisha kwa kutoa maoni yake.

Na kwa hayo yote yali­yofanyika tunaanza kuona taratibu wananchi wame­anza kuelewa zaidi kuhusu sababu za matukio ya ajali za pikipiki, mgawanyiko wake na njia bora za kubore­sha huduma kwa majeruhi wa ajali kwa kadri wanavyo­endelea kufanya tafiti.

Kuhusu watafiti

Kutokana na ukubwa wa changamoto hiyo inayo­tafuna nguvukazi ya Taifa, iliwaleta pamoja wata­fiti kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dk George Kiwango ambaye ali­fanya utafiti katika eneo la ajali za barabarani zitokan­azo na pikipiki na Dk Menti Ndile ambaye yeye amejik­ita katika utafiti wa kuhu­dumia majeruhi wa ajali za barabarani.

Kwa upande wa Dk George Kiwango ambaye alikuwa anafanya utafiti katika Sha­hada ya Uzamili (Master’s Degree) chuoni MUHAS.Anakiri kuwa kufanya kazi na wadau wa masuala ya utafiti wa ajali za barabarani kutoka nje ya nchi, kulibadil­isha mawazo yake na kuan­zia hapo akajikuta anasoma zaidi kuhusiana na ajali za barabarani na kuangalia njia gani ambazo zinaweza kutu­mika kutafutia ufumbuzi.Dk Kiwango anasema hali imebadilika ambapo waendesha pikipiki ndi­yo wamekuwa wahanga wakubwa wa ajali baada ya watembea kwa miguu.

Anathibitisha kuwa hata Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mwanzoni hai­kuwa ikipata majeruhi wa ajali za bodaboda, baadaye ikaanza kupata majeruhi wengi na hapo ndipo ilim­sukuma kujikita zaidi katika utafiti za ajali za pikipiki. Miaka mitatu ilimchukua Dk Kiwango kuufanya na kuu­kamilisha utafiti huu yaani kuanzia 2017-2020.

Kama hiyo haitoshi, aliona mfumo wa usafiri wa pikipiki umekuwa mkubwa na tegemeo la watu wengi na kwa kuwa utaendelea kuwapo kwa miaka mingi hivyo ilimlazimu kutafuta njia za kuboresha ili uwe msaada kwa watumiaji wake ambao wengi ni wananchi wa kawaida.

Kwa upande wa Dk Men­ti Ndile, ambaye ni mtafi­ti na mhadhiri pia kutoka MUHAS, alivutiwa kuchu­kua Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masuala ya uto­aji huduma kwa majeruhi wa ajali za barabarani kutokana na ongezeko la majeruhi na vifo vya ajali za barabarani.

Shahada yake ya uzami­vu aliichukulia MUHAS na Chuo Kikuu cha Umea nchi­ni Sweden kwa kipindi cha miaka minne akishirikiana na mhadhiri msaidizi Gift Lukumay kutoka MUHAS.Anasema matukio ya ajali ya barabarani yamekuwa yakiongezeka na anakiri kuwa Tanzania haijaachwa nyuma.

Dk Ndile anataja moja ya mambo yanayosababisha ajali za barabarani ni hali ya miundombinu. Zingine ni elimu ndogo, kutokuzingatia kanuni za usalama baraba­rani, ongezeko la watu na vyombo vya moto ambalo limekuwa kisababishi cha matukio ya ajali, vyombo vya moto vibovu nk.

“Matukio hayo ya ajali za barabarani ya pikipiki yamesabababisha majeruhi wa ajali kuhitaji rasilimali nyingi kwa ajili ya matiba­bu yao na ikiwa bado kama nchi hatuna rasilimali za kutosha kukidhi matakwa yanayoongezeka kila siku,” anaeleza Dk Ndile.

Watafiti hawa bado ni haz­ina kubwa kwa taifa kwani eneo la ajali za barabarani hususan pikipiki bado ni miongoni mwa maeneo yas­iyofanyiwa tafiti mara kwa mara.

Hitimisho

Kutokana na matokeo ya tafiti, inapendekezwa kuwa­po kwa mikakati mbalim­bali ya kurekebisha tabia na kudhibiti tabia hatarishi miongoni mwa waendesha bodaboda.

Pia, sambamba na hilo, kutokana na ukweli kuwa matumizi ya vilevi yamekuwa sababu kubwa ya matukio ya ajali za boda­boda, hivyo inashauriwa kuwepo kwa njia za kud­hibiti matumizi ya pombe na vilevi vingine kwa ajili ya kuzuia ajali kwa siku za usoni.

Kwa upande wa huduma za tiba kwa majeruhi, ni wakati wa kuhamasisha zaidi tafiti katika eneo hili ili kuona kama huduma zin­azotolewa kwa majeruhi wa ajali za bodaboda zinawa­saidia walau kurejea katika hali zao za kawaida kama si kupona kabis