Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyembaka mjamzito ahukumuwa miaka 30 Jela

Mshtakiwa Agustino Kahise Mkazi wa changalawe akitoka katika Mahakama ya Wilaya ya Mufindi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela kwa kosa la kumbaka mjamazito kwenye choo cha wodi ya wazazi katika hospitali ya Mji Mafinga. Picha na Mary Sanyiwa

Muktasari:

  • Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemuhukumu Agustino Kahise, mkazi wa Changarawe wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 30 Jela, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumbaka mjamazito aliyekuwa amelazwa Hospital ya Mji Mafinga.

Mufindi. Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemuhukumu Agustino Kahise, mkazi wa Changarawe wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 30 Jela, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumbaka mjamazito aliyekuwa amelazwa Hospital ya Mji Mafinga.

Shauri hilo la jinai namba 33, 2023 ambalo hukumu yake imetolewa jana na Hakimu Mkazi Sekela Kyungu.

Akisoma maelekezo yaliyotolewa mahakamani hapo, Kyungu amesema kuwa mnamo April 13, 2023 majira ya usiku katika eneo la choo cha wodi ya wazazi katika hospitali hiyo, bila uhalali mshtakiwa alimbaka msichana huyo (18), bila ridhaa yake.

Aidha Hakimu Kyungu amesema tukio hilo lilitokea baada ya msichana huyo mwenye umri wa mika a 18, kumaliza kujisaidia, na kwamba wakati anatoka chooni kuelekea wodini, ndipo alipokutana na mshtikiwa mlangoni ambaye alimzuia asitoke huku akimziba mdomo kisha kumbaka.

Hakimu huyo amesema Kahise ameshtakiwa kwa kosa la ubakaji ambalo ni kinyume na kifungu namba 130 (1) (2) (e) na kifungu 131(1) cha sheria za kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022.

Hata hivyo aliposomewa shtaka lake, Kahise alikana kutenda kosa hilo ndipo mahakama ikaalika upande wa mashtaka ili waweze kuthibitisha, ambapo waliwasilisha vielelezo viwili pamoja na mashaidi watano.

Kyungu amesema kuwa baada ya ushaidi ambao umetolewa na pande zote mbili, mahakama imeona upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha shtaka hilo bila kuacha shaka yeyote na hivyo ikamtia hatiani kwa kifungu namba 235(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 rejeo la mwaka 2022.

Aidha Hakimu Kyungu ameeleza kuwa, kulingana na kosa ambalo Kahise amelifanya, mahakama hiyo inampa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela chini ya kifungu 131(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022; ili iwe fundisho kwake na watu wenye tabia kama hiyo.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Wakili wa Serikali, Ahmed Magenda, amesema kuwa hakuna kumbukumbu yoyote ya makosa ya jinai kwa mshatakiwa huyo, hata hivyo aliomba mahakama kutoa adhabu kali.

"Niombe Mahakama yako itoe adhabu kali kwa Mshatakiwa ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia kama hiyo, kwa sababu mteja wangu alikuwa katika hali ya kujiuguza lakini mshatakiwa kwa makusudi akamfanyia kitendo hicho cha kinyama," amesema Magenda.