Anayedaiwa kuzini na mwanaye afikishwa mahakamani

Tuesday January 26 2021
Baba aliyebaka pic

Ikwabe Gibogo(58) mkazi wa mtaa wa Chamoto amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuzini na mtoto wake wa miaka 11.

By Anthony Mayunga

Serengeti. Ikwabe Gibogo (58) aliyekamatwa kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake mwenye umri wa miaka 11 amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi  Wilaya ya Serengeti.

Akisoma mashtaka leo Jumanne Januari 26, 2021 mbele ya hakimu Adelina Mzalifu, mwendesha mashtaka  wa Serikali, Paskael Nkenyenge  amesema mshtakiwa huyo wa  kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2021 anakabiliwa na shtaka la kuzini na maharimu.

Amebainisha kuwa Januari 23, 2021 eneo la Chamoto, mtuhumiwa alikamatwa kwa kosa la kuzini na mwanaye  kinyume na kifungu namba 158 (1)(a)  cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2019.

Gibogo alikana mashtaka na kupelekwa mahabusu kesi hiyo ikiahirishwa hadi Februari 9, 2021.

Advertisement