Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anuani za makazi kurahisisha huduma ya zimamoto

Ofisa na Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto Wilaya ya Mufindi, Jackline Mtei akitoa elimu ya majanga ya moto kwa wananchi wilayani hapo kuhusu mfumo wa Anuani za Makazi utakavyosaidia kurahisisha utoaji wa Huduma hiyo. Picha na Mary Sanyiwa

Muktasari:

Mfumo mpya wa anuani za makazi kwa wananchi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa utasaidia kurahisisha utoaji wa huduma mablimbali za kijami ikiwamo zimammtoto.

Mufindi. Imeelezwa kuwa Mfumo wa anuani za makazi kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa utasaidia na kurahisisha namna ya utoaji wa huduma ya majanga ya moto kwa Jeshi la Zimamoto kufika kwa urahisi katika maeneo hayo ili kuweza kudhibiti moto pindi unapotokea.

Hayo yamebainishwa leo na Ofisa na Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto wilayani hapa, Jackline Mtei wakati akizungumza na Mwananchi ofisini kwake kuhusu utoaji wa ya majanga ya moto kwa wananchi wa majumbani, Sokoni pamoja na viwandani wilayani humo.

Amesema mfumo huo wa anuani za makazi utasaidia na kuwarahisishia pindi wanapata taarifa kwa wananchi kuhusu matukio ya moto kuweza kufika kwa wakati tofauti ilivyokuwa sasa.

"Changamoto iliyopo kutokana na kutokuwepo kwa mfumo wa anuani za makazi namna ya mazingira yalivyo asilimia huwa tunatumia vigezo kama mfano shule, Misitiki ,Makanisa na masoko ili kuweza kufika eneo la tukio kudhibiti moto na kufanya uokoaji." amesema Mtei

Mtei amesisitiza kuwa ujio wa mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kujuwa sehemu husika ambako tukio la moto limetokea kwa kutaja namba ya nyumba majina ya mitaa pamoja na barabara ili kuweza kufika kwa urahisi.


Pia ameeleza kuwa kila mwananchi anapaswa kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika maeneo yao ikiwemo Nyumbani,Viwandani ,Shule na Sokoni pamoja na maeneo mengine mbalimbali ya kazi ili kujikinga na majanga hayo

Mkazi wa Mafinga, Prisca Mlelwa amesema kuwa mfumo wa anuani za makazi utasaidia zaidi namna ya utoaji wa taarifa kwa Jeshi la zimamoto pindi majanga ya moto yanapoyokea ili waweze kufika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya uaokoaji.

"Mfumo huo ni mzuri sana kwa sababu utatusaidia kutoa taarifa kwa Jeshi la zimamoto ili waweze kufika kwa urahisi katika maeneo hayo ambayo moto utakuwa umetokea." amesema Mlelwa