Arusha wasitishwa mgomo, nauli mpya zaanza kutumika

Muktasari:
Madereva wa daladala katika Jiji la Arusha wamesitisha mgomo ambao ulianza Leo asubuhi, baada ya kukubalika hoja ya wenye magari kupandisha nauli kwa zaidi ya Sh100.
Arusha. Madereva wa daladala katika Jiji la Arusha wamesitisha mgomo ambao ulianza Leo asubuhi, baada ya kukubalika hoja ya wenye magari kupandisha nauli kwa zaidi ya Sh100.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda kufanya majadiliano na viongozi wa madereva na viongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) katika kituo cha mabasi cha Kilombero.
Mtanda amesema wakati wanasubiri siku 14 zilizotolewa na Latra ili bei kupanda rasmi kwa kuzingatia bei ya mafuta kupanda wamekubali kuanza ongezeko hilo leo.
Leo asubuhi madereva wa daladala katika Jiji hilo walisitisha kutoa huduma na kusababisha adha kkwa wasafiri katika Jiji hilo.
Madereva hao walisitisha huduma wakipinga kuzuiwa kupandisha nauli licha ya bei ya mafuta kupanda.