Babu ashikiliwa kwa madai ya kumbaka mwanafunzi wa miaka 14

Muktasari:
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Abubakar Saidi (64) mkazi wa Kata ya Ndembezi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza (14) katika shule ya sekondari iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga mkoani humo.
Shinyanga. Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Abubakar Saidi (64) mkazi wa Kata ya Ndembezi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza (14) katika shule ya sekondari iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga mkoani humo.
Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 13, 2022 Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Jackson Mwakagonda amedai tukio hilo limetokea Oktoba 10, 2022 saa 8 mchana katika Kata ya Ndembezi.
Kamanda Mwakagonda amedai mtuhumiwa huyo alimrubuni mhanga kwa kumpa Sh10, 000 na kumfanyia ukatili huo.
Aidha Mwakagonda ametoa wito kwa walimu wote kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi hao hali itakayosaidia kupunguza utoro mashuleni.