Bajeti ya Serikali yapitishwa

Friday June 24 2022
bajetipiic
By Sharon Sauwa

Dodoma. Bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023 ya Sh41.48 trilioni imepitishwa na wabunge leo Ijumaa, Juni 24,2022 baada ya wabunge 356 kati ya 379 kupiga kura za ndio.

Akitangaza matokeo bungeni leo Ijumaa Juni 24,2022 Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema jumla ya wabunge 379 waliokuwepo bungeni walipiga kura.

Amesema hakuna mbunge aliyesema hapana huku wabunge 23 wakisema hawana maamuzi.

Waliopiga kura za sina maamuzi ni pamoja na wabunge wa viti maalum waliofukuzwa uanachama na Chadema.

Advertisement