Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi trafiki aonya, akitaja mambo matatu kupiga marufuku namba za 3D

Muktasari:

  • Kila nchi ina chaoa yake ya namba za magari na 2D ni chapa ya Tanzania, hivyo kuibadili kwa kuweka 3D ni kuharibu. Pia namba hizo zinachongwa mitaani bila kibali cha wakala wa kufanya hivyo ambacho hutolewa kwa utaratibu maalumu. Pia zinaweza kutumika kufanya uhalifu, kwani ni rahisi kujitengenezea na kupachika kwenye gari na kuondoa.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani limetaja sababu tatu za kupiga marufuku matumizi ya namba za 3D kwenye magari nchini.
Aidha limeagiza wote walioweka namba hizo kuziondoa kwa hiari kipindi hiki, kabla ya muda wa kuanza kuchukuliwa hatua kufika.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuu wa Usalama Barabara nchini, Ramadhani Ng'anzi amesema wamepiga marufuku namba hizo kwa kuwa zinatengenezwa kiholela mitaani.

"Lakini sababu kubwa ni kwamba, namba hizo sio namba rasmi za nchi yetu,  pia zinaweza kutumika kwenye matukio ya uhalifu.”

Amesema, jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani linaendelea na operesheni ya kuwahimiza wananchi kuziondoa kwa hiari bila kuwachukulia hatua kipindi hiki.

"Kipindi cha hiari kitakapopita, tutakwenda kwenye utekelezaji wa sheria" amesema Kamanda huyo wa usalama barabarani nchini na kuendelea.
"Watu waliobandika namba hizo, wengi tulipowauliza walikiri wakati wanapewa hawakupewa za 3D, waliweka tu wenyewe wanapopajua wao.”

"Tumezipiga marufuku, tumewapa muda wa kuziondoa ni kwa hiari, ingawa Watanzania wengi wanapenda hadi wakamatwe, tunaendelea kuwapa muda wa hiari na hivi karibuni tutatangaza ukomo wa muda huo  kwa kila aliyeweka kuiondoa na  tutakwenda kwenye utekelezaji wa sheria,"amesema.

Amesema, sababu kubwa ya kuzipiga marufuku kwanza namba hizo sio namba rasmi katika nchi ya Tanzania, ambazo ni rasmi ni zile za 2D zilizoidhinishwa na msajili wa magari kupitia mawakala wake.

"Pia namba za 3D haziko kwenye mfumo wa nchi yetu, sababu hazina ubora unaotakiwa, zinatengenezwa na watu ambao hawajaidhinishwa kuwa mawakala wa namba za magari.”

"Hivyo mtu anaweza tu kutengeneza na hata kutumika kwenye uhalifu, tunawahimiza wananchi kuziondoa wenyewe, wafanye haraka iwezekanavyo.
"Kitendo cha kuruhusu namba za magari kutengenezwa huko mtaani kiholela kinaweza kuleta uhalifu, baadhi ya watu wanajitengenezea na kuzipachika kwenye magari na kufanya uhalifu na baadaye kutoweka.

"Baadhi ya waliopachika, katika operesheni ya kuziondoa waliomba tuwape muda wa kuziondoa,

tutaendelea kuzitoa bila adhabu, baada ya kipindi hicho kutakuwa na adhabu," amesema.

Amesema, muda wa hiari ukipita, wale watakaokuwa wanatumia watakamatwa kwa kosa la kuongeza kitu kwenye gari ambacho hakiruhusiwi.

"Ni kama kufoji, kwa kuwa hiyo namba alipewa ikiwa vizuri na yeye kuongeza kitu kingine, ni kama upewe logo kisha wewe uongeze kitu, namba zetu za 2D ni brand (chapa) kufanya tofauti ni kuharibu brand yetu,"amesema.