CRDB yashinda tuzo ya Benki Bora Tanzania

Tuzo ya Euromoney iliyotunukiwa kwa Benki ya CRDB ikiwa imewekwa katika eneo la kuingilia katika ofisi hizo kwa ajili ya wadau mbalimbali kuiona na kupiga nayo picha. Waliosimama na tuzo hiyo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) na viongozi wa juu wa benki ya CRDB.

Muktasari:

Benki ya CRDB inajivunia kutunukiwa tuzo ya Benki Bora nchini kwa mwaka 2022 na Jarida la Euro­money.

Benki ya CRDB inajivunia kutunukiwa tuzo ya Benki Bora nchini kwa mwaka 2022 na Jarida la Euro­money.

Ikiwa ni tuzo yake ya pili kuinyakua, baada ya kush­inda tuzo kama hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2004, ushindi huo haukuwa wa kubahatisha bali jiti­hada na mikakati ya benki hiyo.

Furaha isiyo kifani imemsogeza karibu Mku­rugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nseke­la ambaye anakiri kuwa, “Tuzo ya Euromoney inat­hibitisha nafasi ya CRDB kama benki inayoongoza nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitoa hotuba yake wakati wa kupokea tuzo ya Euromoney kama Benki Bora Tanzania.

Pia inatambua mafanikio ya mageuzi ambayo yame­sababisha ukuaji endelevu wa benki yetu na kunufai­sha wateja wetu, wawekez­aji na uchumi wa nchi kwa ujumla,” Nsekela aliongeza.

Anasema kuwa mafanikio hayo ya katikati ya mwaka yanaakisi mwenendo mzuri wa benki uliowezesha uku­aji endelevu wa tarakimu mbili katika kipindi cha miaka minne iliyopita iki­chagizwa na mageuzi ya kimkakati na uvumbuzi.

Pia anaelezea kuongeze­ka kwa kiwango cha faida cha benki hiyo kwa miaka miwili iliyopita ambapo fai­da baada ya kodi iliongeze­ka kutoka Sh165.2 bilioni mwaka 2020 hadi kufikia Sh268.2 bilioni mwaka 2021.

Hii ndiyo faida kubwa zai­di katika historia ya benki na hiyo inadhihirisha tha­mani ya mageuzi endelevu ambayo benki imeyafanya katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Kulingana na Nsekela, vipimo vingine muhimu vil­ivyoupa ushindi benki hiyo ni uendelevu wa uzalishaji wa thamani kwa wanahi­sa wake (na washikadau wengine) kupitia mapato endelevu.

Pia imekuwa taasisi inay­oongoza kibiashara kusaid­ia minyororo ya thamani ya kiuchumi inayoende­lea kuboresha maisha ya Mtanzania mmoja mmoja na uchumi.

“Katika eneo la ubunifu, benki inaendelea kushika usukani wa soko la Tanza­nia, ubunifu katika kubadil­isha maisha katika sekta ya huduma za fedha katika nyanja ya malipo na bidhaa zilizoboreshwa.

Benki pia inajivunia kuwa kinara katika kutengeneza masuluhisho ya fedha kwa minyororo maalum ya tha­mani kulingana na mpan­go wa uchumi wa nchi,” anaarifu.

Benki hiyo inaonyesha ukubwa wake wa mizania ya Sh 9.4 trilioni kama kicho­cheo chake cha kiuchumi mbali na kuwezesha sekta muhimu za uchumi kama vile; kilimo, miundombinu, viwanda na utalii, miongoni mwa mambo mengine.

Mafanikio ya Benki ya CRDB vilevile yanachagiz­wa na kampuni yake tanzu ya CRDB Burundi ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika biashara yake katika kipindi cha miaka 10 toka kuanzishwa kwake.

“Benki itaendelea kutanua wigo wake na hivi karibuni inatarajia kuin­gia katika soko la Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) kurahisisha ufanyi­kaji wa biashara baina ya Tanzania na DRC ukizinga­tia nchi hiyo inategemea bandari ya Dar es Salaam kwa uuzaji na ununuaji wa bidhaa,” anafafanua zaidi.

Kwa upande mwingine, Nsekela anaeleza kuwa Benki ya CRDB ni benki ya kwanza ya biashara Afrika Mashariki iliyoidhinishwa na Mfuko wa Hali ya Hewa ya Kijani (GCF) kama taasisi mwezeshaji wa uboreshaji wa mazingira nchini.

Akielezea zaidi kauli hiyo hapo juu, anasema kuwa pia ni Taasisi ya kwanza mion­goni mwa zile zilizochaguli­wa na Mfuko wa GCF kupata kibali cha ufadhili wa mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi na teknolojia ya kilimo unaolenga kubore­sha kaya zaidi ya milioni sita Tanzania.

Pia, Benki ya CRDB ni balozi wa masuala ya maz­ingira nchini kupitia Mradi wa ‘Pendezesha Tanzania’ ambao unalenga kutunza mazingira kupitia upandaji miti, usafi wa miji na nishati endelevu.

Nini maana ya Euromoney?

Euromoney ni jarida la kimataifa linalochanganua data kutoka kwa kampuni zote duniani na kutam­bua biashara zinazofanya vizuri zaidi ikiwemo benki za biashara.

Euromoney imekuwa ikifanyia tathmini taasisi za fedha zinazoongoza ulimwenguni kupitia tak­wimu za kiutendaji, tafiti na tuzo ilizowahi kushin­da kwa zaidi ya miaka 25 katika eneo la huduma za kibenki.

Tuzo za kila Mwaka za Ubora (AAEP), zilianzish­wa mwaka 1992 na kuvutia ushiriki wa zaidi ya benki 1,200 viongozi duniani kote. Tuzo hizo zinatambua ubora katika vipengele vya kimataifa, kikanda na nchi binafsi.

Vijana wanaofanya gwaride wakipokelewa kwa furaha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya CRDB, Profesa Neema Mori, Meneja wa Ushirikiano wa Kimkakati wa CRDB, Masele Msita na wafanyakazi wengine wa benki ya CRDB wakati tuzo hiyo ikiwasili katika lango kuu la benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.

Euromoney ipo katika zaidi ya nchi 160 na zaidi ya wafanyakazi 2,500 walio Amerika Kaskazini, Ameri­ka Kusini, Ulaya na Asia.

Namna utaratibu ulivyoku­wa?

Pamoja na jukumu lake la kupima na kutunuku tuzo za ubora wa benki, kamati ya Tuzo hizo za AAEP ilifan­ya mapitio ya utendaji wa benki hiyo, dhidi ya mkakati wake na eneo ambalo benki hiyo inaendesha shughuli zake ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki.

Utengenezaji wa tha­mani wa benki na mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania na Burundi pia uliiongezea alama benki hiyo katika kinyang’anyiro hiko.

Ushindi huu una maana gani kwa Benki ya CRDB?

Hatua iliyofikiwa ina­maanisha uwepo wa ari ya hali ya juu ya benki katika kuchochea ukuaji zaidi unaosimamiwa na mikakati thabiti na ya kimaendeleo iliyopangwa na benki.

Ni fursa ya benki kuji­weka karibu zaidi na dunia, kutanua wigo wa bidhaa, ushiriki wa jamii na uvum­buzi wa hali ya juu.

Benki ya CRDB inajivu­nia mafanikio hayo lakini haiwezi kubweteka kwa hatua na badala yake ni mwanzo wa safari nyingine ya mafanikio zaidi.