Dar, Kilimanjaro zaongoza wenye ‘viriba tumbo’

Muktasari:

  • Kilimanjaro, Zanzibar na Dar es Salam zaongoza kwa watu wenye uzito mkubwa na viliba tumbo huku hali ya lishe kwa watoto waliochini ya miaka mitano ikiwa hairidhishi hasa kwa Mkoa wa Iringa, Njombe na Rukwa.

Mtwara. Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa tatizo la uzito uliozidi na kiriba tumbo limekuwa janga la kitafa katika mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam, Unguja na Mjini Magharibi huku udumavu nao ukishika kasi katika mikoa ya Iringa, Njombe na Rukwa.

 Akizungumza leo Jumamosi Aprili mosi wakati akizindua mbio za Mwenge kitaifa alisema kuwa tatizo la kiliba tumbo ni kubwa katika mikoa ya Kilimanjaro  kwa asilimia 49, Dar es salaam kwa asilimia 48.6,  Unguja kwa asilimia 39.4 na Magharibi kwa asilimia 47.4 hali hii inaelekea kuwa janga kitaifa.

Huku utapia mlo ukiwa katika mikoa ya Iringa 56.9, Mbeya 31.5, na Njombe 50.4 Rukwa 49.8 Geita 38.6, Ruvuma 35.6, Kagera 34.3, Simiyu 33.2 Tabora  33.1, Katavi 32.2, Manyara 32, Songwe 31.1.

“Hali hii ya watu kuwa na uzito ulizidi ni janga la kitaifa na kisababishi cha kuongezeka kwa magonjwa kama ya moyo na kisukari, saratani nafikiri ni wakati mwafaka wa kubadili mtindo wa maisha kwa kufanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku pamoja na na kula mlo kamili na kupunguza pombe, mafuta na sigara,”  amesema Waziri Mkuu.

“Lishe kila binadamu anahitaji kula chakula bora na cha kutosha kwa kula vyakula vya Mizizi, jamii ya kunde, mbogamboga, matunda, asali, sukari vyakula hivi vitasaidia kuondokana na hali ya lishe isiyoridhishi kutokana na watoto chini ya miaka mitano kuathiriwa na hali hiyo,” amesema.

“Nawasihi wakuu wa mikoa haya yakafanyiwe kazi hali ya lishe iliyozidi ndio kiashiria ambacho hakijawahi kupungua ambapo kimeongezeka kutoka asilimia 11.3 hadi asilimia31.7 kwa mwaka 2018.