Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Ubungo aagiza kuondolewa mkuu wa ulinzi NIT

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James (wa kwanza kulia) akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) hawapo pichani.

Muktasari:

Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James ameagiza kuondolewa kwa Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi kutoka Suma JKT katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kutokana na taarifa za unyanyasaji wa wanafunzi wa taasisi hiyo.

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James ameagiza kuodolewa kwa Mkuu wa Kitengo cha ulinzi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SumaJKT), katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

James ameagiza kuondolewa kwa mkuu huyo kufuatia kusambaa kwa video mbili mitandaoni vikionesha askari wa Suma JKT wanaosimamia ulinzi na usalama NIT, wakipigana na mwanafunzi pamoja na mtoa huduma ya chakula chuoni hapo kitendo ambacho amedai ni udhalilishaji.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo leo Januari 21, jijini hapa wakati wa kikao kilichokuwa kikijadili video hizo za udhalilishaji wa wanafunzi uliyofanywa na askari hao wa Suma JKT.


Amesema pamoja na uongozi wa Suma JKT kuwachukulia hatua za kinidhamu askari waliohusika na vitendo hivyo, anaagiza kuondolewa pia kwa Mkuu wa Kitendo hicho chuoni hapo.

“Uongozi wa Suma JKT wamuondoe huyo mkuu wa kitengo ambaye alikuwa akisimamia ulinzi chuoni hapo, nataka aondoke na yeye kama walivyoondolewa askari wale wengine waliofanya makosa, aletwe mkuu mpya na askari wengine wapya ili wasimamie makubaliano ambayo yamewekwa sasa,” amesema.

Amesema Suma JKT kwa kipindi hiki ambacho bado wameaminiwa kuwa walinzi wa chuo hicho, ni lazima wahakikishe askari wanaowaleta hapo ni wale wenye weledi, wanayoyaishi maadili ya ulinzi lakini wanaoheshimu utu wa mtu na taratibu zilizowekwa katika taasisi ya umma.

“Endapo likatokea tukio lingine katika eneo hili  na ikabainika limesababishwa na askari, tutakielekeza chuo hiki kifanye mbadala wa mkataba na chombo kingine cha ulinzi,” amesema.

Awali akifafanua matukio yaliyotokea chuoni hapo, James amesema mara baada ya kufika NIT walibaini ukweli wa matukio yaliyosambaa mitandaoni yalifanyika ambapo tukio la kwanza ni la mwanafunzi ambaye alizuiliwa kuingia chuoni kwa sababu hakuwa na kitambulisho.

“Na huo ndio utaratibu wa chuo hiki kuwa mtu asiyekuwa na kitambulisho haruhusiwi kuingia kwa sababu za kiusalama walizojiwekea hivyo mvutano uliyotokea baina yake na askari ulitokana na mwanafunzi huyo kukaidi amri ya kutokuingia bila kuwa na kitambuliko,” amesema

Amesema katika tukio la pili lilikuwa ni baina ya askari wa Suma JKT na mwanamama anayefanya kazi ya kutoa huduma ya chakula chuoni hapo ambapo alizuiliwa kwa sababu alikuja muda ambao sio wa kazi na alivaa mavazi ambayo hayaruhusiwi chuoni hapo.


“Kwa hiyo katika kuzuiliwa kwake akaingia kwenye mvutano mkubwa na askari na video yake ikasambaa katika mitandao ya kijamii, pamoja na kwamba askari walikuwa wakitekeleza majukumu yao lakini namna ambayo walidili na watu hao wawili haikubalikii,” amesema.

Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Wanafunzi NIT, Jeremiah Stephen amemkuru DC Kheri kwa kufika chuo hapo na kutoa maagizo kwa lengo la wanafunzi kuwa katika hali ya usalama.

“Niwahakikishie kwamba wanafunzi wapo katika hali ya usalama na matukio hyao yameshatatuliwa na kwa sasa vijana wanaendelea vema na mitihani yao,” amesema

Naye Rais wa Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu nchini (TAHLISO), Frank Nkinda amesema video hizo zilizua taharuki kwa wazazi na watanzania kwa ujumla lakini kupitia kikao cha leo wamejua kilichosababisha na hatua tayari zimeshachukuliwa.