Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DED Buhigwe asimamishwa, Waziri Kairuki asema…

Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki 

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe (DED), mkoani Kigoma, Essau Ngoloka amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, ikiwa ni siku chache zipite tangu Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango kueleza kutoridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya hiyo.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe (DED) mkoani Kigoma, Essau Ngoloka kupisha uchunguzi.

Mkurugenzi huyo amesimamishwa ikiwa ni siku chache zimepita tangu, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aeleze kutoridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Buhigwe.

Dk Mpango alisema anazo taarifa za baadhi ya miradi utekelezaji wake haufanani na fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi hiyo na kwamba hawezi kukubaliana na hali hiyo, ni lazima waliosababisha wawajibishwe.

Leo Jumanne Julai 11, 2023, taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Tamisemi, Nteghenjwa Hoseah imeeleza Waziri Kairuki amechukua hatua hiyo baada ya mkurugenzi huyo kushindwa kudhibiti matumizi ya fedha ya miradi ya maendeleo.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari Kahimba ambayo ilipelekewa fedha Sh1 bilioni, hata hivyo mradi huo haujakamilika na fedha zote zimetumika.

 “Kutokana na tuhuma hizo, Waziri Kairuki amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, kuunda timu ya uchunguzi ya matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Buhigwe na kuwasilisha taarifa kwake,” amesema Nteghenjwa

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kairuki amewataka wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za mitaa kote nchini kuendelea kusimamia vyema miradi ya maendeleo na kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa utekelezaji wa miradi, zinakamilisha miradi husika kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha.