Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DED Ruangwa mbioni kuwakatia wakulima bima za afya

Watumishi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Frank Chonya (mwenye tisheti jeupe). Picha na Bahati Mwatesa

Ruangwa. Halmashauri ya Ruangwa, mkoani Lindi inatarajia kuanza kwa mchakato wa kuwakatia bima ya afya wakulima wake katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili wapate huduma hiyo kwa uharaka na kukuza tija katika ufanyaji kazi.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Agosti 24, 2023 na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Frank Chonya katika maonesho ya wiki ya madini na uwekezaji yanayo fanyika katika viwanja vya  soko jipya wilayani hapa.

"Tutawakatia bima ya afya hata ya mwaka mmoja mmoja kwasababu wakulima wetu wanapopata fedha hawawezi kukumbuka kukata bima ya afya na anapougua anapata shida, bima ya afya itamsaidia kupata huduma kwa haraka,"amesema Chonya.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi, Irene Kataraiya ametoa rai kwa wakulima na wananchi kujitokeza kwa wingi kukata bima hiyo kwa manufaa yao.

"Ugonjwa hautoi taarifa, jiungeni na NHIF kwa ajili ya kupata huduma bora za afya na ukishakata bima utaanza kuitumia ndani ya siku 30," amesema Irine

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagi akiongea katika maonyesho hayo amewaomba NHIF wayafikie makundi mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini.

Mayasa Goloa, mkazi wa Ruangwa amesema kuwa Serikali ikiamua kukata fedha moja kwa moja kwa mkulima baada ya kuuza mazao itakuwa vizuri zaidi kwasababu wengi hujisahau wakishapata fedha.