Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond ajitosa vita dawa za kulevya, ashauri vijana kuachana nayo

Msanii wa Muziki Tanzania, Nassib Abdul maarufu 'Diamond Platnumz'

Muktasari:

  • Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz ametumia jukwaa la kilele cha maadhimisho ya kitaifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya yanayofanyika jijini Arusha, kukemea vitendo vya vijana kujiingiza katika matumizi ya mihadarati ikiwemo dawa za kulevya.

Arusha. Nyota wa muziki wa kizazi kipya Afrika, Nasibu Abdul maarufu Diamond Platnumz ameingia kwenye vita ya kupambano kwa kuwataka vijana nchini, kuachana matumizi ya dawa za kulevya kwani hazina manufaa yoyote katika maisha yao.

Diamond amezungumza hayo katika maadhimisho ya kitaifa ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid  leo Jumapili, Juni 25, 2023 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema matumizi ya dawa za kulevya licha ya kuharibu afya pia uvutaji unaondoka fursa kwa vijana.

"Ukiwa unatumia dawa za kulevya unaitwa teja hakuna ambaye atakupa kazi, hakuna ambaye atakupokea hata katika muziki sisi tukikuona tunakuona teja tu," amesema.

Amesema hakuna faida yoyote katika dawa za kulevya na matumizi yake yanaondoa ndoto za kuishi vizuri wala kuaminiwa katika jamii ikiwepo kupata kazi.

"Leo mimi nimetoka Tandale nimefika Arusha kwa sababu naaminiwa," amesema Diamond.

Ujumbe huo wa Diamond ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wasafi Media, ulishangiliwa na mamia ya watu ambao wanashiriki katika maadhimisho hayo.