Diamond na Nandy wachukua tena tuzo

Monday December 21 2020
nandpic

Dar es Salaam. Wasanii wa Tanzania, Diamond Platnumz na Nandy wameshinda tuzo za wasanii bora Afrika zilizotolewa na Aeausa.

Mbali na wawili hao kuibuka na ushindi, msanii Rayvanny ameshinda tuzo ya msanii bora Afrika Mashariki, Kusini na Kati  huku DJ Sinyorita akishinda tuzo ya DJ bora.

Ushindi huo unawafanya Nandy na Diamond kuwa na  tuzo mbili za kimataifa mwaka 2020 baada ya kushinda tuzo za Afrimma Novemba, 2020  katika vipengele cha msanii bora wa kiume na kike Afrika Mashariki.

Rayvanny na DJ Sinyorita tuzo hizo ni za kwanza kwao mwaka 2020.

Tuzo za Aeausa (Africa Entertiment Award USA)  zilifanyika kwa njia ya mtandao na kurushwa kupitia chaneli yao ya Youtube.

Tuzo hizo zilizoanzishwa mwaka 2015 na Waafrika wanaoishi nje ya bara hilo kwa ajili ya kuwatunuku tuzo wasanii wa Afrika,

Advertisement

hushindanisha watoa burudani hasa wa barani Afrika na huwa na vipengele 30.Advertisement