Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mpango aongoza mapokezi ya Kardinali Rugambwa

Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhadhama Protase Rugambwa akiwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango.

Muktasari:

  • Siku nane tangu Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhadhama Protase Rugambwa kusimikwa hadhi hiyo ya ukadinali, amewasili nchini leo ambapo mapokezi yake yameongozwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango.

Dar es Salaam. Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhadhama Protase Rugambwa, amewasili nchini leo baada ya kusimikwa hadhi ya ukadinali ambapo mapokezi yake yameongozwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango.

Dk Mpango aliambatana na viongozi wa Kanisa Katoliki akiwemo Kardinali Polycap Pengo, aliyekuwa Waziri wa Nyumba na Makazi William Lukuvi pamoja na viongozi wengine wa kidini na kisiasa.

Mbali na viongozi hao wa kidini waumini wa Kanisa Katoliki nao walijitokeza kumlaki kiongozi huyo huku wakiimba nyimbo za pongezi.

Waumini waliovalia sare, walianzisha ngoma na nyimbo karibu na eneo la kupokea watu mashuhuri katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Wakati shangwe za kumlaki kiongozi huyo zikiiendelea, Makamu wa Rais Dk Mpango aliongozana na Kadinali Rugambwa kwenye chumba maalumu na kufanya mazungumzo na baada ya mazungumzo mafupi Rugambwa alielekea Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Rugambwa amewasili nchini leo Septemba 6, 2023 akitokea nchini Italia akihudhuria misa takatifu ya kusimikwa ukardinali.

Katika misa ya kumsimika ukadinali Askofu Rugambwa iliongozwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis.

Rugambwa alipata hadhi hiyo akiwa na wenzake 21 katika misa maalum iliyofanyika Vatican ambako ni makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani.

Kwa hatua hiyo, Rugambwa anakuwa mtu wa tatu nchini, kuwa na hadhi hiyo akitanguliwa na Laurean Rugambwa aliyefariki Disemba 1997 na Kardinali Polycap Pengo aliyestaafu Uaskofu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam mwaka 2019.

Baada ya Kardinali kusimikwa hadhi hiyo Septemba 29, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wake wa X aliandika: “Hongera sana Mwadhama Protase Rugambwa, Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo kuu Katoliki Tabora kwa kupata hadhi ya ukardinali.”

Ameongeza kuwa "Pongezi za dhati kwa Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, kwa kusimikwa rasmi na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Kardinali. Kauli mbiu ya utume wako ni ‘Enendeni ulimwenguni kote,’ ikiakisi mafundisho ya Yesu Kristo katika Injili ya Marko 16:15, juu ya utume unaojali watu wote, sehemu zote na wakati wote. Naungana na Watanzania wote kukuombea kheri, afya njema, na mafanikio katika utumishi wako.”